na mimi nimekumbuka mbali, nilijua gari zao ni pickup tu, kumbe zipo saloon pia.
miaka hiyo mtu mwenye gari pickup aidha ana toyota hilux pickup au datsun pickup.
Hivi Datsun na Nissan sio kampuni moja?
Wachaga wameuvamia uzi huu wakidhani ni mapick up. Wachaga kwa Datsun.
mbona kama kivitz. lol.
Dah Umenikumbusha long mkuu Datsun Gari letu la pili mzee alinunua baada ya kuwasota sana na mgongo wa Chura... Datsun 120Y Warejeshe na Morris pia tumezimiss gari niliyokuwa napenda Maishani
mkuu wacha tu tuuvamie huu uzi,kuna gari ambazo mchaga hatakaa azisahau kizazi chake chote
1- bedford- hii ndio kama fuso ya enzi hizo kabla ya isuzu injection tx hazijaingia, bodi yake ilikuwa ya mbao .sijui kizazi cha fuso kinayajua haya
2- pioget pickup na sedan
3- toyota stauti- dume na jike
4- mandolini- landrover ya handeli- hii unashusha injini unafanya mashine ya kusagia kisha unairudisha unaenda kubebea mbege kibosho