David Kafulila Alisema Ukweli kuwa CCM Inabadilika kulingana na wakati na mahitaji ya wakati

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa David Kafulila Kamishina wa PPP,Msomi wa BBA,Kijana Mchapa kazi,mzalendo , muadilifu na akili kubwa amewahi kusema ya kuwa CCM inabadilika kulingana na wakati na mahitaji ya wakati . akaendelea kusema ya kuwa ndio maana huwezi ukawakusanya wapinzani wa CCM kutoka Mfumo wa vyama vingi na kuwaweka pamoja .

Kiukweli maneno na kauli ya Mheshimiwa Kafulila zinaendelea kujidhihilisha na kuonyesha ukweli na uhalisia. Ni kweli kabisa kuwa CCM imekuwa ikijisahihisha ,kubadilika kulingana na Wakati na mahitaji ya kila kundi na rika. Imekuwa na usikivu wa kusikiliza sauti za watu na nini zinahitaji.

Ndio maana hufikia wakati wapinzani wanakosa ajenda na sera za kwenda nazo kwa wananchi ,kwa kuwa kile kinachokuwa kilikuwa ajenda kuu ya upinzani kinakuwa kimetekelezwa na kufanyiwa kazi na CCM. Lakini pia kitendo na hatua ya CCM kuja na sura mpya ya Mkuu wa Nchi yaani Rais kila baada ya miaka kumi,Nacho kimekuwa kikileta taswira mpya, Matumaini,matokeo chanya na kukata kiu ya watu.

Embu angalia kutoka utawala wa Hayati Benjamini Mkapa,Mzee Daktari Jakaya Mrisho Kikwete, Hayati Dkt John Pombe Magufuli na sasa Mheshimiwa Jemedari Daktari Samia Suluhu Hasssan.Ukiangalia aina ya uongozi wa viongozi hao utakuta kila mmoja alikuwa na aina yake ya uongozi.

Ndio maana unaweza kukuta aliyekuwa mpinzani mkuu wa Hayati Dkt John Magufuli akaja kuwa rafiki wa Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hasssan,lakini pia unakuta aliye kuwa mpinzani Mkuu wa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akaja kuwa na urafiki na maelewano na Hayati Daktari John Magufuli.

Mfano Dkt Slaa wa wakati wa Mheshimiwa Dkt Kikwete alibadilika na kuwa tofauti na dkt Slaa yule wa wakati wa Hayati Dkt Magufuli, Mheshimiwa Zitto Kabwe wa wakati wa Dkt Jakaya Kikwete hakuwa Zitto yule wa wakati wa Hayati Dkt Magufuli. Angalia wapinzani kuanzia 1992 utakuta wengi sana walishahama kutoka upinzani na kujiunga CCM chama kilichobeba matumaini ya watanzania na chenye uchungu na maisha ya watanzania.

Hata leo unapoona Mheshimiwa Mchungaji peter Msigwa anajiunga CCM ni matokeo ya hicho alichokieleza na kukisema Mheshimiwa David Kafulila.Kikubwa ni kufahamu kuwa CCM ni dude moja kubwa sana ambalo halishikiki na huwezi ukashindana nalo na ukashinda

Ni dude kubwa lililo na mfumo imara na madhubuti na lenye kujiendesha kitaasisi na lenye intelligensia kali sana kama ilivyo CIA na FBI za Marekani mashirika ya ujasusi na upelelezi.Ndio maana hakuna chama cha Upinzani kinachoweza kupanga kitu au mkakati wowote ule ukawa siri kwa CCM.CCM ipo kila mahali na kila sehemu.mkono wa CCM ni mrefu sana kama ilivyo Mossad ya islael.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Nasikia Umebubujikwa na machozi ya furaha baada ya Kamishina wa TRA kuenguliwa na kuteuliwa wa ZRA.

Wewe ni Mtanganyika wa kweli
 
Ndiyo maana sasa hivi imebadilika inatetea ufisadi kupitia spika Tulia
 
Nasikia Umebubujikwa na machozi ya furaha baada ya Kamishina wa TRA kuenguliwa na kuteuliwa wa ZRA.

Wewe ni Mtanganyika wa kweli
Acha ujinga wako hapa. Tanzania ni moja na sote ni watanzania.kamishina mpya amewahi pia kuwa Diwani Dar. Na ni mtu wa Mbeya .
 
Back
Top Bottom