Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Jumla ya miradi ya maendeleo 84 inatekelezwa kwa ubia baina ya sekta binafsi na Serikali kupitia kituo cha ubia Kati ya Seikali na Sekta binafsi (PPPC) kikieleza miradi miwili ya Barabara za kulipia ikiwemo ile ya Kibaha hadi Morogoro pamoja na Barabara za mzunguko za kulipia katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa mbioni kuanza kutekelezwa.
Akizungumza Jijiji Dar es Salaam wakati wa semina na madiwani kutoka wilaya ya ilemela Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia cha Serikali na sekta binafsi David Kafulila, amesema miradi hiyo ipo ambayo imeshaanza kutekelezwa na kuleta faida kama vile miradi miwili ya Bandari huku miradi ya Barabara ya kulipia ikiwemo ya barabara ya mzunguko ya kulipia itakayojengwa Jijini Dsm ikitegemewa kusaidia kupunguza foleni.