David livingstone alipona vipi porini Afrika

David livingstone alipona vipi porini Afrika

Superpower

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2018
Posts
826
Reaction score
920
Unajua huwa najiuliza Sana.Afrika ambako ni nyumbani kwa wanyama wakali Kama vile nyoka wakali Kama koboko, mamba, simba, chui na magonjwa ya kitropikia Kama malaria. Sasa huwa najiuliza huyu jamaa alizunguka vp mapori ya kipindi hicho bila kuuwawa na wanyama wakali au kuugua
 
Very simple.Alitumia wenyeji katika shughuli zake na hawa walikuwa na uelewa mkubwa wa mazingira yao.La pili Ulaya ilishakuwa na muingiliano na mataifa kama ya Amerika kusini ambapo hali almost sawa na ya Africa.Kuna mambo walipata huko pamoja na magamba ya cinchona kama dawa ya malaria.
 
Nimesoma biography ya Henry Morton Stanley, kama unamkumbuka poa. Yeye alikua ni mwandishi wa habari wa NEW YORK TIMES na alikuja Africa kumtafuta Dr.Livingtone baada ya kupotea mawasiliano nae kwa muda mrefu sana. Hawa jamaa, yani inisikitisha sana. Watu waliowasaidia kutembea humu Africa ni sisi wenyewe. Walikua wakifika Zanzibar, wanaenda kwa wazawa basi wanasaidia kuwatafutia watu wa kwenda nao Bara. Kama bwana huyo Stanley yeye marayake ya kwanza alitoka Bagamoyo na msafara wa watu Takribani 600. Nakurudi Zanzibar baadae na na watu chini ya 200. walikua wanapata shida sana. Ila kama tusingewasaidi yani mpaka leo kungekua hakuna cha ukoloni wala nini. Ni sisi wenyewe ujinga wetu.
 
Tumesoma shule ya msingi lengo la safari ya Livingstone Afrika ilikuwa kutafuta chanzo cha mto Nile. Hivi inawezekana alikuwa na agenda ya siri zaidi ya kutafuta chanzo mto?
 
Very simple.Alitumia wenyeji katika shughuli zake na hawa walikuwa na uelewa mkubwa wa mazingira yao.La pili Ulaya ilishakuwa na muingiliano na mataifa kama ya Amerika kusini ambapo hali almost sawa na ya Africa.Kuna mambo walipata huko pamoja na magamba ya cinchona kama dawa ya malaria.
shukrani nilikua najiuliza Sana dawa ya malaria before ya mseto na qunine
 
Unajua huwa najiuliza Sana.Afrika ambako ni nyumbani kwa wanyama wakali Kama vile nyoka wakali Kama koboko, mamba, simba, chui na magonjwa ya kitropikia Kama malaria. Sasa huwa najiuliza huyu jamaa alizunguka vp mapori ya kipindi hicho bila kuuwawa na wanyama wakali au kuugua
Nadhani unafahamu chanzo cha kifo chake ni malaria.
 
Nadhani unafahamu chanzo cha kifo chake ni malaria.
but alikua ameshatembea Sana. Lazima alikua ana dawa sema Kuna jamaa kaongelea magamba ya cinchona ambayo ni kweli yalikua yana tibu pia ni source ya quinine hadi leo
 
Unajua huwa najiuliza Sana.Afrika ambako ni nyumbani kwa wanyama wakali Kama vile nyoka wakali Kama koboko, mamba, simba, chui na magonjwa ya kitropikia Kama malaria. Sasa huwa najiuliza huyu jamaa alizunguka vp mapori ya kipindi hicho bila kuuwawa na wanyama wakali au kuugua

Dr. David Livingstone - Mmishionari Mpelelezi, alikuwa ni Tabibu kwa taaluma! Lengo lake kubwa ni kwenda kufanya Umisheni na Upelelezi CHINA,lakini Robert Moffat Mmishionari aliyekuwa akifanya huduma Afrika Kusini ndiye aliyemshawishi kuja kufanya Mambo yake Afrika baada ya kupewa michapo mingi ya kusisimua juu ya Afrika.

Kwanza kabisa alikuwa akitembea na wenyeji wa bara hili la afrika ambao walijua mazingira yao vizuri.
Wenyeji hawa walimsaidia Kubeba shehena yake ya Dawa na Vitu vingine alivyovihitaji safarini.Pia walimsaidia katika Mawasiliano kwa Lugha za Kiafrika katika maeneo mbali mbali(Translators).

Kwa mfano Livingstone aliongozana na Wasaidizi wake Waaminifu sana SUSI na CHUMA.
Aliwafundisha mambo mengi sana ikiwa pamoja na kuhifadhi maiti isioze na ndivyo walivyofanya kwa mwili wake alipokufa.

Pili alijenga mahusiano mazuri na Wenyeji wa Afrika kwa kufikia kwa Watawala (CHIEFS) na Hawa walitoa Msaada mkubwa kwa Wageni.
Mfano alipokuwa maeneo ya Swaziland au Zimbabwe kama nakumbuka vema alijeruhiwa vibaya sana na Simba hivyo isingekuwa wenyeji wa maeneo hayo angekufa! Walimtibu na kumsaidia mpaka pale alipopona kabisa na kuendelea na safari yake.
 
Back
Top Bottom