David Mataka wa ATCL, ahukumiwa kulipa faini Tsh milioni 8 kwa kulisababishia hasara ya Tsh Bilioni 71 shirika

Ndo upumbavu huu sasa nini milioni 8 kwa b 71 kwann asipigwe risasi tu kama China
 
Kesho ataiba tena b 120 akijua atalipa milioni 12
 
Siku zote nasema Hakuna wa kumfunga fisadi TANZANIA, jela ni kwa ajili ya watu masikini wasio na pesa za kununua UHURU wao
 
Halafu Kuna watu wanatupigia kelele kila siku suala la Uzalendo.........ndiyo maana mtu anang'oa miundo mbinu ya reli au barabara na kwenda kuuza vyuma chakavu hawana tofauti na huyu mtaka kabisa ila hukumu zao lazima zitofautiane
 
Uzalendo ni kichaka cha kuwapumbazia wajinga
 
Sheria za TANZANIA hukumu yako itategemea na kiasi cha pesa ulizoiba ukiiba kidogo utafungwa miaka mingi , ukiiba nyingi utalipa faini kidogo uamuzi ni wako.

 
Fisadi aliyeifilisi nssf akazawadiwa ubalozi Malasyia akale bata pattaya beach
 
Mpaka anapigwa hiyo faini ya Million8 hapo ashohonga kama million50 kuweka mambo sawa...
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…