Davina Akiri Kuwa Waigizaji Wengi wa Kike Wanajiuza

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906

Muigizaji mkongwe wa filamu na moja kati ya waasisi wa Kaone Sanaa Group, Halima Yahya ‘Davina' amekiri kuwa ndani ya tasnia yao, kuna waigizaji wengi wa kike wanajiuza kwa maslahi yao binafsi.

Akipiga stori na paparazi wa GPL, Davina alisema wasanii wanaofanya hivyo ni wale wasio na nia ya dhati, wapo kwenye tasnia kwa ajili ya kuuza sura na kujinadi kwa mapedeshee.

"Tatizo ni kwamba wasanii tumekutana kila mmoja ana tabia zake na ni ngumu kujua undani wa mtu kwa kumtazama mara moja, sasa utakuta mtu yupo radhi aombe kucheza filamu hata bure kwa kuamini kwamba ataonwa na wanaume wenye pesa zao, na kweli inakuwa hivyo kwani wanapowatokea hawakatai, kimsingi wanatuchafua sana sisi ambao tupo serious na kazi," alisema Davina.

Chanzo:GPL
 
Ila Mtoto mzuri huyu...sijui nae fail lake lipoje duh!
 
Hawa wasanii bana...wote wakihojiwa wanasema wenzao ndio wanajiuza..nina wasiwasi hawajui maana ya kujiuza so inabidi waulizaji wabadili namna ya kuuliza.
 
Hili sinia (tasnia )ya bongo movie khatari wanawake wanaishi kwa hisani ya mapedejee! wanamume wengine nao wanaishi kwa hisani ya mapedejee! sielewi elewi kwa kweli jamani.
 
Hata hapo ofisini kwenu wanauza pia msiwaone wasanii malaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…