Uchaguzi 2020 Davis Mosha: Mpeni Magufuli, hao wengine watauza nchi

zanku

Member
Joined
Jun 9, 2020
Posts
70
Reaction score
152
Aliyewahi kuwa Mgombea wa CCM Moshi Mjini na bilione Davis Mosha amwombea kura, Rais Magufuli, Priscuss Tarimo na Juma Raibu


Kada wa Chama cha Mapinduzi na Aliyekua Mgombea wa Ubunge Moshi Mjini 2015, Ndugu Davis Mosha leo aliendelea na Kazi ya Kuomba kura za Urais kwa Dr. John Pombe Magufuli, Kura za Ubunge kwa Priscus Tarimo na Kura za Madiwani wa CCM. Davis Mosha alikutana na Kinamama vijana na Wazee wa Kata ya Miembeni katika Kikao cha ndani na kuzungumza nao Umuhimu wa Kuipa kura chama cha Mapinduzi.

Pia alitumi nafasi hiyo kueleza kazi alizozifanya Dr. John Pombe Magufuli pamoja faida ya kumchagua katika Kipindi kingene cha Miaka mitano.

Aliwasihi wakina mama na Wazee kuzungumza na Vijana wao juu ya Mustakabali wa Maisha yao ya Baadae kwani kura yao ni yenye thamani kubwa na Dr. Magufuli pekee ndiye anayeweza kuipa thamani kura hiyo.

ia alitumia muda huo kumuombea Priscus Tarimo kura za Ubunge na kuahidi iwapo Priscus atachaguliwa basi atatekeleza zile ahadi binafsi alizoahidi mwaka 2015 kupitia Priscus na Madiwani wake. Davis Mosha alimaliza kwa kusema bado nia yake ni kukombolewa kwa Jimbo la Moshi ili tupate maendeleo.View attachment 1605388View attachment 1605389View attachment 1605390


View attachment 1605436
 
Vipi, alikumbuka kuwaeleza ndege zimeanza kulalia! Awalete waje wazione kwenye banda lao, na mshiko aliwapa buku tano au aliwaongeza cha juu.
 
Huyo ndio Davis Mosha bhana😛😛😛😛
 
Davis Mosha rafiki yangu wa zamani soma upepo
 
Reactions: BAK
Kama yeye alivyotaka kuiuza yanga, utajiri wake ni uuzaji nchi mtupu
 
Atufafanulie nchi inauzwaje? Maana Somalia pamoja na kuwa ilikuwa haina serikali lakini haijawahi kuuzwa!
 
Atupe mfano wa nchi ambayo ilishawahi kuuzwa na kwa nani ikiwezekana atupe na mkataba pamoja na risiti ya EFD ya mauziano kama hana hiyo ni propaganda tu kama zilivyo nyingine
 
Huyo davis ni yahaya anaishi wapi Moshi ilimkataa anabwela maskini tu pesa zake za magumashi
 
Hapa hajawasaidia lolote anaowaombea kura, vinginevyo ana hofu ya hao watu wake kukosa kura toka kwa ccm wenzake.

Sasa kikao cha ndan lzm kihudhuriwe na maccm so it is nonsense, hii ingekuwa na mashiko kama angeenda nje ya wanaccm labda kwa chadema kuomba kura na si ktk kikao cha ndani... overrrrr
 
Tusidanganyike !Maendeleo ni Mchakato, yapo mengi aliyofanya Rais wetu na Tunajivunia kua na Rais Mazalendo na Mchapakazi kama Dr.Magufuli ..Tunaendelea Nae...!KURA KWA MAGUFULI
#ChaguaMagufuli
#ChaguaMagufuli
#ChaguaMagufuli
#ChaguaMagufuli
#ChaguaMagufuli
#ChaguaMagufuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…