Dawa bandia za kutibu TB zadaiwa kuingizwa nchini

Dawa bandia za kutibu TB zadaiwa kuingizwa nchini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
TB+pic.jpg


KWA UFUPI
DAWA bandia zinazodaiwa kutibu ugonjwa wa kifua kikuu (TB), zinahofiwa kuingia nchini, ambapo zinadaiwa kutumika kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili tangu mwaka 2011.

DAWA bandia zinazodaiwa kutibu ugonjwa wa kifua kikuu (TB), zinahofiwa kuingia nchini, ambapo zinadaiwa kutumika kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili tangu mwaka 2011.

Dawa hizo zinazodaiwa kusambaa katika miji mikubwa ya Afrika, zinadaiwa kuanza kuleta madhara kwa watumiaji kwani hazina uwezo wa kuua wadudu wanaosababisha ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wakaguzi kutoka Marekani,dawa hizo aina ya Rifampicin, Antibiotics simesambaa katika miji 19 na 7 nchi zilinunua dawa hizo.

Aidha utafiti huo unaonyesha kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa TB ambapo asilimia 6.6 ya Afrika, asilimia 10.1 India na 3.9 asilimia katika Brazil, China, Thailand, Uturuki na Urusi watu milioni tisa duniani kote huugua TB.

Miji iliyotajwa kununua dawa hizo bandia ni pamoja na Luanda(Angola),Sao Paulo(Brazil), Beijing(China), Lubumbashi(DRC)na Cairo(Misri). Miji mingine ni Addis Ababa(Ethiopia), Accra (Ghana), Dar es Salaam(Tanzania), Delhi na Kalkata(India),Nairobi(Kenya),Lagos(Nigeria),Moscow(Urusi),Kigali(Rwanda),Bangkok( Thailand) ,Istanbul(Uturuki),Kampala(Uganda) na Lusaka(Zambia).

Utafiti huo unaeleza pia kwamba,dawa hizo zinashindwa kufanya kazi kwa asilimia 16.6 asilimia kwa upande wa Afrika, asilimia 10.1 katika India na 3.9 asilimia katika Brazil, China, Thailand, Uturuki na Urusi.

Kauli ya TFDA

Akizungumza na gazeti hili ili kuthibitisha taarifa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Hiit Sillo alisema kwa sasa hana taarifa yoyote kuhusiana na kuingia kwa dawa hizo bandia nchini.

Mkurugenzi huyo alilitaka gazeti hili kumtafuta Ofisa Uhusinao wa TFDA kwa taarifa zaidi,kwani yeye hayupo kazini kwa kipindi cha wiki moja kwa hiyo asingeweza kutoa ufafanuzi wa suala hilo.

“Siwezi kuzungumza chochote kwani sina taarifa hizo,ila mnaweza kumtafuta Ofisa Uhusiano kwa majibu zaidi mimi nipo nyumbani kwa wiki moja sasa naumwa. Pia sina taarifa juu ya suala hilo,”alisema Sillo.

Gazeti hili lilimtafuta Ofisa Uhusiano wa TFDA,Gaudensia Simwanza ambapo alisema taarifa hizo hazina ukweli,kwani kila wakati wanafanya utafiti ili kutambua dawa bandia na hakuna dawa za kifua kiuu ambazo zimejulikana kama ni bandia kama inavyodaiwa.

Alisema kwa kawaida dawa za kifua kikuu haziuzwi na badala yake zinatolewa bure sasa kupatikana kwa dawa bandia ni kitu ambacho hakiwezekani kwani zinatolewa kwa umakini mkubwa. “Kwanza ni vyema ikafahamika kwamba dawa za kifua kikuu haziuzwi kwani zinatolewa bure na hazitakiwi kuuzwa, sasa tunashangaa kusikia dawa hizo zimesambaa nchini kwa kipindi cha miaka mwili,”alisema Simwanza.
Alisema TFDA ina utaratibu wa kufanya utafiti wa dawa mbalimbali ikiwa pamoja na dawa za kifua kikuu ambapo kwa kipindi cha mwaka 2011/12 dawa zote za kifua kikuu zilifanyiwa ukaguzi na hakuna dawa iliyotambulika kuwa ni bandia.

“Tunautaratibu wa kufanya ukaguzi wa dawa mbalimbali,ambapo mwaka jana na mwaka juzi tulifanya ukaguzi wa dawa zote za kifua kikuu na hakuna dawa ambazo zilikutwa ni bandia kama inavyodaiwa. Sasa taarifa kama hizo sio za kweli na Watanzania wasiwe na wasiwasi,”alisema.chanzo.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1688526/-/item/0/-/raendr/-/index.html



 
TB+pic.jpg


KWA
UFUPI

DAWA bandia zinazodaiwa kutibu
ugonjwa wa kifua kikuu (TB), zinahofiwa kuingia nchini, ambapo zinadaiwa
kutumika kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili tangu mwaka 2011.

DAWA bandia
zinazodaiwa kutibu ugonjwa wa kifua kikuu (TB), zinahofiwa kuingia
nchini, ambapo zinadaiwa kutumika kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili
tangu mwaka 2011.


Dawa hizo zinazodaiwa
kusambaa katika miji mikubwa ya Afrika, zinadaiwa kuanza kuleta madhara
kwa watumiaji kwani hazina uwezo wa kuua wadudu wanaosababisha ugonjwa
huo.


Kwa mujibu wa utafiti
uliofanywa na wakaguzi kutoka Marekani,dawa hizo aina ya Rifampicin,
Antibiotics simesambaa katika miji 19 na 7 nchi zilinunua dawa
hizo.


Aidha utafiti huo
unaonyesha kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa TB ambapo
asilimia 6.6 ya Afrika, asilimia 10.1 India na 3.9 asilimia katika
Brazil, China, Thailand, Uturuki na Urusi watu milioni tisa duniani kote
huugua TB.


Miji iliyotajwa kununua
dawa hizo bandia ni pamoja na Luanda(Angola),Sao Paulo(Brazil),
Beijing(China), Lubumbashi(DRC)na Cairo(Misri). Miji mingine ni Addis
Ababa(Ethiopia), Accra (Ghana), Dar es Salaam(Tanzania), Delhi na
Kalkata(India),Nairobi(Kenya),Lagos(Nigeria),Moscow(Urusi),Kigali(Rwanda),Bangkok(
Thailand) ,Istanbul(Uturuki),Kampala(Uganda) na Lusaka(Zambia).


Utafiti huo unaeleza pia
kwamba,dawa hizo zinashindwa kufanya kazi kwa asilimia 16.6 asilimia kwa
upande wa Afrika, asilimia 10.1 katika India na 3.9 asilimia katika
Brazil, China, Thailand, Uturuki na Urusi.


Kauli ya TFDA

Akizungumza na gazeti hili
ili kuthibitisha taarifa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na
Dawa(TFDA), Hiit Sillo alisema kwa sasa hana taarifa yoyote kuhusiana na
kuingia kwa dawa hizo bandia nchini.


Mkurugenzi huyo alilitaka
gazeti hili kumtafuta Ofisa Uhusinao wa TFDA kwa taarifa zaidi,kwani
yeye hayupo kazini kwa kipindi cha wiki moja kwa hiyo asingeweza kutoa
ufafanuzi wa suala hilo.


“Siwezi kuzungumza chochote
kwani sina taarifa hizo,ila mnaweza kumtafuta Ofisa Uhusiano kwa majibu
zaidi mimi nipo nyumbani kwa wiki moja sasa naumwa. Pia sina taarifa
juu ya suala hilo,”alisema Sillo.


Gazeti hili lilimtafuta
Ofisa Uhusiano wa TFDA,Gaudensia Simwanza ambapo alisema taarifa hizo
hazina ukweli,kwani kila wakati wanafanya utafiti ili kutambua dawa
bandia na hakuna dawa za kifua kiuu ambazo zimejulikana kama ni bandia
kama inavyodaiwa.


Alisema kwa kawaida dawa za
kifua kikuu haziuzwi na badala yake zinatolewa bure sasa kupatikana kwa
dawa bandia ni kitu ambacho hakiwezekani kwani zinatolewa kwa umakini
mkubwa. “Kwanza ni vyema ikafahamika kwamba dawa za kifua kikuu
haziuzwi kwani zinatolewa bure na hazitakiwi kuuzwa, sasa tunashangaa
kusikia dawa hizo zimesambaa nchini kwa kipindi cha miaka mwili,”alisema
Simwanza.

Alisema TFDA ina utaratibu wa kufanya utafiti wa dawa mbalimbali
ikiwa pamoja na dawa za kifua kikuu ambapo kwa kipindi cha mwaka
2011/12 dawa zote za kifua kikuu zilifanyiwa ukaguzi na hakuna dawa
iliyotambulika kuwa ni bandia.


“Tunautaratibu wa kufanya ukaguzi wa dawa mbalimbali,ambapo
mwaka jana na mwaka juzi tulifanya ukaguzi wa dawa zote za kifua kikuu
na hakuna dawa ambazo zilikutwa ni bandia kama inavyodaiwa. Sasa taarifa
kama hizo sio za kweli na Watanzania wasiwe na
wasiwasi,”alisema.chanzo.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1688526/-/item/0/-/raendr/-/index.html[FONT=Times
New Roman]



[/FONT]

Mkuu,kinachonishangaza hzi dawa huwa haziuzwi,hutolewa bure,sasa wanaleta dawa fake kwa maslahi yapi,au shida yao wagonjwa wote wafe,watengenezaji wa hzo dawa hawana nia nzuri na maisha ya waafrika,ni vema kampuni itakayogundulika kutengeneza hzo dawa isusiwe kununua product yake yoyote ile
 
Arv nazo si zinagawiwa bure-? Mbona zilinunuliwa fake? Ishu hapo ni waagizaji wa msd ndo tatizo kubwa humu nchini. Wanajali matumbo yao zaidi kuliko afya za wagonjwa wetu. Ukifuatilia siku hizi wagonjwa wanaokuwa diagnosed na tb wanatibiwa na kuugua tena ndani ya miezi michache. Are we doing wrong diagnosis au wagonjwa hawatumii dawa au dawa fake?
 
Dawa za tb zinanunuliwa.tatizo ni wanunuz wa izo dawa kuleta nchini.wananunua za rahisi ili wachikichie mshiko madhara yake ndo haya sasa.ii sisi wenyewe na si wazungu
 
Kwa nini mnaanza kulaumu wazungu wakati Mkurugenzi wa TFDA anasema hajui?hata msemaji wao amesema hakuna dawa feki na anashangaa eti kuwa zimekuwepo nchini kama miaka miwili!Tunapaswa tuwaulize kuhusu taarifa ya kuwepo dawa hizo wameifanyiaje kazi ama wameipuuza na kwa nini wameipuuza?Mi naongeza hata dawa za malaria wakifanya utafiti huenda wakapiga marufuku kabisa kwani hazitibu vizuri!
 
Mkuu,kinachonishangaza hzi dawa huwa haziuzwi,hutolewa bure,sasa wanaleta dawa fake kwa maslahi yapi,au shida yao wagonjwa wote wafe,watengenezaji wa hzo dawa hawana nia nzuri na maisha ya waafrika,ni vema kampuni itakayogundulika kutengeneza hzo dawa isusiwe kununua product yake yoyote ile
nadhani kuna maslahi kwa wanaoziingiza si kwa watoaji kwa mtumiaji wa mwisho!!ni kweli zinatolewa bure kwa wagonjwa je serikali inapewa bure huko zitokako?huenda zinanunuliwa kwa bei ndogoooo kwa vile ni fake halafu zina andikiwa kiasi kukubwa cha fedha kama vile si fake!!
 
Back
Top Bottom