Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,261
Unaumwa kichwa cha kupasuka, unaenda kwenye akiba yako ya dawa na kukuta Aspirin, bahati mbaya fungashio lake laonesha dawa hii ime-expire miaka miwili iliyopita. Je, utatumia ama utaacha? Ukiamua kutumia hii aspirin litakuwa ni kosa kubwa au utaamua kutotumia na kuendelea kupata maumivu makali ya kichwa? Huu ni mtanziko unaowakumba wagonjwa wengi.
Ni kweli ile alama ya expiration date (ED) huwa inamaanisha kitu, lakini yamkini si ile maana tuijuayo sote. Toka sheria zilipoanza kupitishwa miaka ya sabini, watengenezaji wa dawa wanatakiwa kuweka alama ya expiration date katika bidhaa zao. Hii ni tarehe ambayo mtengenezaji bado anaweza akakuhakikishia utendaji kazi na usalama wa dawa husika kwa asilimia mia.
Kisheria, watengeneza dawa hawahusiki na matatizo yatakayotokana na matumizi ya dawa baada ya expiration date. Pia mara tu, kifungashio cha dawa original kinapofunguliwa, ama na mgonjwa au mtumishi wa afya, expiration date iliyoandikwa kwenye kifungashio haitahusika tena.
Elimu kubwa kuhusiana na tarehe yak ku-expire dawa, zinatokana na tafiti zilizofanywa Marekani na Mamlaka ya Dawa na Chakula (FDA) baada ya kuombwa na jeshi la Marekani. Jeshi likiwa na akiba kubwa ya dawa zenye gharama kubwa, lilihitajika kubadirisha dawa kila baada ya miaka michache. Lakini FDA wakagundua kwamba 90% ya zaidi ya dawa aina 100 zilizohifadhiwa, zilikuwa ni nzuri hata miaka 15 baada ya tarehe ya ku-expire (wastani ilikuwa miezi 66 baada ya Expiration Date). Mojawapo ya dawa zilizoonwa bado zinafanya kazi vyema na salama baada ya tarehe ya expiry ni pamoja na amoxicillin, ciprofloxacin, diphenhydramine, na morphine. Hizi dawa zilikuwa bado ni bora toka tarehe ya expiry kwa miezi 12 hadi 184 ya ziada.
Mwaka 2001 American Medical Association (AMA) walitoa taarifa kwamba dawa nyingi bado zinakuwa salama na zikali na nguvu zaidi ya ile tarehe iliyoandikwa ya ku-expire. Taarifa yao hiyo nayo iliegemea kwenye matokea ya FDA waliyofanya dhidi ya dawa za jeshi la Marekani.
Lakini ni vigumu kwa mteja au mtumishi wa afya kujua dawa ipi inaweza ikawa bado ni salama na inatenda kazi vyema baada ya expiration date.Uwezekano wa dawa kuwa bado bora baada ya tarehe ya ku0expire utategemea kiasi cha dawa zilizomo ndani ya dawa husika, mwanga, unyevunyevu, mabadiriko ya joto na vitu vinginevyo vihusuvyo uhifadhi bora, na kubwa ni kwa dawa kuwa katika kifungashio original.
Hivyo expiration date haioneshi kwamba hapo ni kikomo cha dawa kufanya kazi au kwamba dawa haiko salama kutumika. Mamlaka za tiba zinatambua kwamba dawa zilizo expire ni salama kutumika hata kama zime expire miaka kadhaa iliyopita. Lakini kwa nadra sana hili si sahihi kwa dawa ya tetracycline, japo watafiti bado wanabishana. Ni kweli kwamba utendaji kazi wa dawa unaweza pungua jinsi siku zijongeavyo, lakini sehemu kubwa ya utendaji kazi wa dawa unakuwapo bado hata miaka kumi baada ya dawa ku-expire. Lakini hapa ukiziondoa dawa kama Insulin, antibiotics za maji, ila dawa nyingi zinafanya kazi kwa muda mrefu sawasawa na jeshi la Marekani lilivyogundua.
Dawa ambazo ziko katika mfumo wa vidonge, zinaonesha kwamba ndizo huweza kuhifadhi ubora zaidi hata baada ya expiration date.
Kama dawa inahitajika, na mgonjwa hawezi kupata dawa nyingine zaidi ya ile iliyo expire na pia hakuna ushahidi kwamba si salama kutumia dawa husika basi waweza tumia. Lakini ikiwa dawa hii ni kwa ajili ya kutibu magonjwa sugu kama ya moyo, kifafa, allergy, yamkini ni hekima ukitafuta dawa ambazo expiration date bado haijapita.
Kama dawa iliyo expiry ni kwa ajili ya magonjwa madogo madogo kama kuumwa kichwa, unaweza ukatumia, japo utendaji kazi wake unaweza usiwe wa asilimia mia.
Ikiwa dawa iliyo expiry itatumika, na mgonjwa akagundua dawa haitibu vizuri, ni vyema dawa ikabadirishwa na nyingine. Lakini jambo kubwa kuliko lote ni kuwasiliana na daktari wako unapokuwa na shaka.
Lakini watu wasisahau pia kuwa expiration date inawasaidia watengenezaji wa dawa. Dawa ikisha expire inakula kwako, hivyo ni lazima ukanunue nyingine. Ila pia inasaidia kuwafanya wenye viwanda kutengeneza dawa mpya na labda zenye formulations tofauti lakini zilizo bora. Kukosekana kwa nguvu ya dawa, ni hatari, hususani pale unapotibu bakteria, ambapo ni rahisi kutengeneza bakteria sugu.

Kwa Msaada wa machapisho kadhaa…