Hapo chini ndiyo habari yenyewe ati. Na hiyo dawa haina jina kwa hiyo imeitwa "Viagra mpya" Lol....Habari yenyewe haina nukuu wala jina la mtaalam au wataalam waliohusika na huo unaodaiwa kuwa uvumbuzi. Halafu mijitu humu na akili zao inanunua habari kama hizi.
Wanasayansi Wavumbua Viagra Mpya ya Kupaka
Vidonge vya Viagra Wednesday, September 23, 2009 8:17 AM
Wanasayansi nchini Marekani wamevumbua dawa mpya ya kuongeza nguvu za kiume kama losheni inayopakwa kwenye uume na wamesema kuwa dawa hiyo mpya haina madhara yoyote mwilini na huanza kufanya kazi sekunde chache baada ya kupakwa kwenye uume.Tofauti na vidonge vya kuongeza nguvu za kiume aina ya viagra ambavyo husababisha madhara mwilini, wanasayansi wamevumbua dawa mpya ya kuongeza nguvu za kiume ambayo hupakwa kwenye uume na haina madhara yoyote mwilini.
Viagra hiyo mpya ambayo ipo kama losheni imeonyesha mafanikio na huanza kufanya kazi sekunde chache baada ya kupakwa kwenye uume tofauti na vidonge vya Viagra ambavyo baada ya kumezwa mwanaume hulazimika kusubiri nusu saa ndio shughuli ianze.
Matatizo ya kutosimama vyema kwa uume huwatokea wanaume wengi duniani huku takwimu zikionyesha kuwa mwanaume mmoja katika kila wanaume 10 nchini Uingereza anakabiliwa na tatizo hilo wakati nchini Australia hali ni mbaya zaidi kwani mwanaume mmoja katika kila wanaume watano anakabiliwa na tatizo hilo.
Vidonge vya viagra humsaidia mwanaume kuwa na ufanisi zaidi kitandani kwa kuifanya mishipa ya damu itanuke na kupelekea kuongezeka kwa mzunguko wa damu mwilini.
Viagra huifanikisha hali hiyo kwa kuvizuia vimeng'enyo vya phosphodiesterase type 5 kufanya kazi zake hali ambayo husababisha madhara mbali mbali mwilini kama vile maumivu ya kichwa, matatizo ya macho, ubongo na matatizo mengine makubwa mwilini.
Lakini dawa hii mpya ya kuongeza nguvu za kiume iliyovumbuliwa na wanasayansi toka chuo kikuu cha Yeshiva University, New York, haina madhara yoyote na ilionyesha mafanikio makubwa ya hapo hapo ilipotumiwa.
Katika majaribio waliyofanyiwa panya, viagra hiyo mpya ilionyesha mafanikio makubwa kwa panya tisa kati ya kumi waliofanyiwa majaribio.
Wanasayansi walisema kuwa matokeo ya majaribio hayo kwa panya hayawezi kutofautiana na matokeo ya majaribio hayo kwa binadamu