Dawa murua ya mti Shamba ya kutibu kikohozi

Dawa murua ya mti Shamba ya kutibu kikohozi

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Jana wakati napitia Uzi mmoja kuhusu yiba za asili,nikambuka marehemu Bibi yangu.

Utotoni Bibi alionionesha mti fulani ambao ukisikia kikohozi unakata kipande unakipitisha kwenye Moto unatafuna na kumeza maji yake. Ukifanya hivi Mara tatu kwa siku kikohozi kinakata. Nakumbuka nilikuwa nikitafuna baada ya dk chache nahisi sukari mdomoni...hakika dawa hii haikuwahi niangusha!

Bahati mbaya itakuwa ngumu kwa wasomaji wote kuelewa kes kuwa Bibi aliniambia jina lake kilugha kinyiramba unaitwa MtumbaKigulu, Kigulu maana yake Ni kichiguu...na mti huu unaota Sana kwenye maeneo ya mfinyanzi karibu na kichuguu! Huu mti Ni evergreen na Ni rahisi Sana kuutambua nyakati za kiangazi

Kwa aliyeko Iramba na maeneo yanayofanana jiografia na Iramba ukisikia kikohozi hebu kakate kitawi kidogo Cha mti huu, pitisha kwenye Moto Kama dakika Kama Dakika mbili tafuna meza maji yake utaona matokeo.

Wazee wetu walikuwa na Ilimu pana Sana bahati mbaya tulikuwa tunachukulia poa!
 
Mimi najua hii kwetu huko..
imgres.jpg
 
Angalieni msije mkalisha watu miti yenye Sumu
 
Back
Top Bottom