Dawa ya Asma

kuna dawa flani hivi ya kienyeji zaidi inatengenezwa hivi;
Mahitaji:
Yai (la kuku wa kienyeji)
pili pili manga ya unga(iliyosagwa)
Asali.
Matayarisho:
chukua pili pili manga vijiko vitatu vya chakula, Chukua asali vijiko ishirini vya chakula, changanya kwenye pili pili manga kisha chukua kiini cha yai changanya kwenye mchanganyiko huo.
Dozi:
kijiko kimoja cha chakula X3 kwa siku 7.
Jaribu hiyo mkuu ni dawa nzuri sana ambayo haina effects kiafya kwani vitu vyote hivyo ni natural.
 
 
HTML:

Mkuu asantesana nimeelewa maelekezo yako ninatengeneza huo mchanganyo nakuanza dos
UBARIKIWE MKUU
 
Pole sana mkuu, i know how yo feeling. you r not alone in this. at least ww ni mmoja. mm nina wawili wote wana asthma. one is 3years boy na 1year baby girl. huwa wanapata attack mpaka wanawekwa kwenye nebulizer(electrical device). wanatumia inhalers zinaitwa asthalin na budecort. zinawasaidia sana.

last month nilikwenda pale muhimbili kitengo cha tiba asili wakanipa dawa naona kama imewasaidia maana frequency ya kupata attacks imepungua.

ni hospitali gani walidiagnos hiyo kitu? walimpima vipimo gani?
 
Pole kwa mwanao.

Ponda kitunguu sumu punje mbili na changanya kwenye nusu glasi ya maziwa moto, weka asali mbichi kijiko kikubwa kimoja, mpe hivyo asubuhi anapoamka na siku kabla ya kulala. Pia chunguza mazingira yanayosababisha apate shambulio au vyakula na vinywaji. Hakikisha hawi na njaa kwa muda mrefu na pia asivimbiwe ama kula kupita kiasi hasa vyakula vyenye gesi. Mungu atamsaidia.

nb. pia dawa ya Ndg. Ndibalema ni sahihi. waweza tumia zote hakuna shida kwa sababu ni chakula.
 
muone mzizimkavu atakusaidia
Asante Mkuu Preta Mungu akubariki
preta nipe namba yake
namba yangu ni hii +905427150528 nipo nje ya nchi lakini.
 
kwanza naomba kutoa masikitikitiko yangu kutokana na baadhi ya michango ambayo imetolewa hapa.Mtu anapoumwa/anapouguliwa anakuwa na mfadhaiko na wakati mwingine anaweza akafuata ushauri hata wa kipumbavu na ndio maana watu wanatumia mambo ya ajabu na unaweza kushangaa kwani wengine ni watu walio na elimu zao.
Napenda nikushauri nikiwa ni daktari.
Pumu ni kubana kwa njia ya hewa kunakotokana na mwili kukabiliana na hali ambayo inasababisha utoaji wa kemikali zinazosababisha njia ya hewa ibane.
Mara nyingi ugonjwa huu unarithika kwa maana ya kuwa kama kwenye familia kuna mtu mwenye ugonjwa huu kuna uwezekano mkubwa kwa watoto kupata.
Hakuna matibabu ya kuponyesha ila kama unajua kinacho anzisha (ainna ya vumbi fulani,perfume etc) na ukakiepuka vinginevyo ni lazima utumie dawa za kukupa nafuu kama salbutamol,aminophyline na jamii ya steroid.Nakushauri usipoteze pesa zako bali fuatilia matibabu ya hpspitali kwa ukamilifu.
USIJARIBU BANGI!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…