Dawa ya babu wa loliondo yatia mashaka

kibajaj

Senior Member
Joined
Apr 12, 2011
Posts
106
Reaction score
26
Daktari mkuu wa mkoa wa arusha asubuhii hii amethibitisha kuwa dawa ya babu huyo inasemekana kuponya magonjwa sugu ni utata mtupu kwani hakuna mgonjwa ambaye mpaka sasa amethibitika kupona. Dr Shiture Salehe Akiongea mbele ya watafiti wa kimataifa waliopo mkoani humo amasema dawa hiyo haina uponyaji ambao watu wanasema hasa katika gonjwa la ukimwi. na kwa upande wa kisukari amasema ni dawa nyingi za kienyeji zinazoonyesha kutibu magonjwa hayo kitaalamu
Amesema hayo akitoa taarifa ya watafiti wa kimataifa waliopo mkoani humo kuichunguza dawa hiyo.Je tumuachie mungu au au tuendelee na uchunguzi au hawa ni wale waliovunja masharti ya babu
 
Common sense makes Sense.... inakuwaje Mungu atoe adhabu kwa wagonjwa dunia nzima wafuate tiba LOLIONDO?, MUNGU hawezi kuwa hivyo, nguvu na masharti ya Babu ni SATANIC!
 

Kikombe cha babu ni Placebo...nashangaa kwanini hajakamatwa mpaka leo anaendelea kutapeli watu kwa kigezo cha imani?
 
Mbona na viongozi wetu walipiga kikombe karibu wote? Hakuna anaweza kututhibishia hapa jamani kuwa yuko fiti?
 
Kikombe cha babu ni Placebo...nashangaa kwanini hajakamatwa mpaka leo anaendelea kutapeli watu kwa kigezo cha imani?
AKAMATWE? Babu anaheshimika kuliko Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO) , ana enjoy huduma (nyingi zinagaramiwa na serikali) ambazo RMO hawezi kuzipata
1. Ulinzi wa Polisi-kulinda utaratibu wa tiba na amani
2. Walinzi na wasaidizi binafsi
3. Ana simu za mkononi za kampuni tatu na anaingiziwa airtime
4. Ana maafisa habari binafsi- full time
5. Anafanya biashara ya kimataifa bila leseni wala kulipa kodi
6. Ana full acess ya kuonana na PM, PRES, Mawaziri bila mizengwe

Kwa ujummla huyu babu ni wakala wa serikali katika mambo ya tiba mbadala, lakini kiimani anadalili zote za kuwa ni kuwa ni wakala wa SHETAN.
 
Je, kuna wagonjwa waliokunywa dawa ya babu ambao sasa ni wazima kabisa, hawana matatizo yoyote ya kiafya?
 
Babu akamatwe mara moja na afikishwe mahakamani kwa mauwaji ya watu na ulaghai wa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
 
mauza uza tu hakuna kikombe wala nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…