Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson Jumanne Juni 16, amewashukuru wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Oxford kwa kugundua dawa ambayo inaweza kupatikana kwa bei nafuu ya paundi tano za Uingereza na kupunguza vifo vya COVID kwa kiasi kikubwa.
Mganga Mkuu wa England Professor Chris Whitty amesema kuwa majaribio ya dawa hiyo yataokoa maisha ya watu duniani kote kwa kuwa Dexamethasone inapatikana katika kill nchi kwa bei nafuu zaidi ya bei ya Uingereza.
Ifahamike kuwa Chuo Kikuu cha Oxford hakijavumbua dawa ya Dexamethasone na kwamba wanasayansi wa chuo hicho wamegundua kuwa dawa hiyo ambayo ilivumbuliwa zaidi ya make 60 iliyopita na ambayo inatumika duniani nzima inaweza pia kutumika katika matibabu ya COVID-19. Wanasayansi wanasisitiza kuwa Dexamethasone inapunguza vifo kwa wagonjwa wa COVID-19 wanaopatiwa hewa ya oksijeni tu kwa kutumia mashine.
Profesa Peter Horby mwanasayansi aliyesimamia utafiti huo amesema kuwa dawa hiyo inapunguza hatari ya vifo kwa wagonjwa hao kwa asilimia 35. Na kwa wanaoongezewa oksijeni bila mashine maalum vifo vinapungua kwa asilimia 20.
Hata hivyo utafiti wa Oxford unaonesha kuwa Dexamethasone haiwasaidii wagonjwa ambao wana dalili tu za maambukizi ya virusi hivyo.
Dawa ya itagharimu dola 50 za Marekani ($50) kwa kuwatibia wagonjwa wanane.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeipongeza Uingereza kwa utafiti huo. Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, WHO Director-General amesema kuwa hii ni dawa ya kwanza inayoonesha kuwa itapunguza hatari ya vifo kwa wagonjwa wanaotumia oksijeni kwa mashine au bila mashine.
“Hizi ni taarifa muhimu na ninaipongeza serikali ya Uingereza na Chuo Kikuu cha Oxford, hospitali nyingi na wagonjwa ambao wameshiriki katika mafanikio makubwa ya kisayansi ya kuokoa maisha ya watu", amesema Dr, Tedros Adhanom Ghebreyesus wa WHO, Jumatano Juni 16, 2020.
Dexamethasone ni dawa gani?
Jambo la kwanza, ni muhimu kuwa kuwa dawa siyo mpya na kwamba ilivumbuliwa na wanasayansi mwaka 1957 baada ya majaribio kwa wagonjwa mbali mbali ikagundulika kuwa inaweza kutumika kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wenye aleji kali kama vile uvimbe unaotokana na maji yanayojaa kwenye misuli mwilini, ugonjwa wa tumbo na aina fulani za kiharusi.
Miaka minne badae ya najaribio mengi zaidi Dexamethasone iliruhusiwa na Shirika la Afya Duniani kutumika rasmi kwa matibabu ya changamoto hizo za kiafya katika mwaka wa 1961.
Sindano ya Dexamethasone ambayo ni jamii ya corticosteroids, inatumika kwa ajili ya kudhibiti magonjwa yanayotokana na aleji ya damu, ngozi, macho, tezi ya shingo (Thyroid), figo, mapafu na mfumo wa mishipa ya fahamu.
Jambo la pili ni muhimu kutambua kuwa Dexamethasone siyo tiba wala chanjo ya COVID-19. Na ndio mana haifai kutumiwa na watu ambao wana dalili tu za korona au wagonjwa ambao hawaongezewi hewa ya oksijeni kwa mashine au la.
Je, dawa hii ni kweli inapatikana katika nchi zote na hasa zile zinazoendelea kama Tanzania? Hili ni swali ambao litajibiwa na wataalamu ya dawa za binadamu, watafiti wa dawa, taasisi mbali mbali za dawa na utafiti wa tiba za magonjwa ya binadamu na hospitali zetu nchini.