manchoso
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 1,605
- 2,055
Mti huu sio mgeni kwa tiba kwa baadhi ya nchi za Africa, siku za nyuma pia ulikuwa ukitumika kutibu malaria na maradhi mengine madogo madogo, Madascar wameendelea kugawa bure na kuhamasisha wananchi kutumia dawa hiyo
Sio mti kama mti unaotibu covid 19 bali wenyewe wanachanganya na baadhi ya mitishamba yao ya kaisili na wameipa dawa hii jina la COVID ORGANICS ambayo taarifa kutoka kwa Rais wa Madascar Andry Rajoelina anasema utengenezaji wake uimegawanyika katika sehemu mbili: kuna ambayo inatibu covid 19 na ambayo inazuia covid 19,
Mnamo tarehe 1/5/2020 serikali ya Equatorial Guinea ilituma wawakilishi kwenda kuchukua dawa hiyo na Madagascar imefungua milango kwa nchi nyingine za Africa kwenda kuchukua na kutumia dawa hiyo kwa wananchi,
Japokuwa kuna upinzani kutoka nchi za magharibi juu ya usalama wa dawa hii, na hii bila shaka imetokana na kuwa watu wa magharibi wanaamini Africa sio sehemu ya kupata tiba bali ni sehemu ya vita maradhi na umasikini {huu ndo ukweli}
Ikiwa basi dawa hii itafanikiwa itakuwa ni maendeleo makubwa kwa bara la Africa na bila shaka itatupa kujiamini waafrica kwamba tunaweza kupambana na majanga kwa kutumia tiba zetu za asili {ambazo kwa hakika ndo tiiba sahihi kwa maradhi yeyote yanaomsumbua mwanadamu ] na litaionesha dunia kwamba Africa inaweza ikawa suluhisho la matatizo makubwa kama hili la maradhi ya corona yanayosumbua dunia,
Jamii forum
Be the first to know