Wapendwa wadau heshima kwenu. Kuna wengine ndani ya jukwaa chili ndo mwanzo mwisho wa matatizo mbalimbali kiafya. Naombeni kujuzwa dawa ya kichomi upande wa kushoto jamani, inanisumbua kwa siku nne mfululizo nimetumia antibiotic lakini hola. Inauma kiasu kwamba kusimama upright in
shida hata kuvuta pumzi, kulala maumivu makali.
Natanguliza shukrani za dhati
TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO
Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya.
Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi chunguza zaidi.
Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.
- Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi
- Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic
Jambo la kuangalia ni je?
- Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?
- Umeinama au umelala
- Ukishakula chakula
Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.
Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa
wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimengenyui sawasawa linachoka.
Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan
usiweke pilipili katika kila mlo.
Tatizo jingine ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana. Chumvi inakorofisha pia
mzunguko wa damu mwilini.
Hasa kama hunywi maji.