Dawa ya kichomi

Lamchina

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Posts
240
Reaction score
120
Wapendwa wadau heshima kwenu. Kuna wengine ndani ya jukwaa chili ndo mwanzo mwisho wa matatizo mbalimbali kiafya. Naombeni kujuzwa dawa ya kichomi upande wa kushoto jamani, inanisumbua kwa siku nne mfululizo nimetumia antibiotic lakini hola. Inauma kiasu kwamba kusimama upright ni shida hata kuvuta pumzi, kulala maumivu makali.

Natanguliza shukrani za dhati.
 
Kaka si vema kutumia dawa bila ushauri wa daktari. Nakushauri fika hospital kwa ushauri zaidi na uchunguzi wa kina.
 
Acha kumzingua mkuu. dawa ni mafuta ya taa tu paka sehemu husika ndani ya sekunde kadhaa utakuwa Poa

Saluti kwako uyui kwetu! I was looking for the same thing! much respect mkuu! stay blessed
 
Me kichomi kikinishika huwa napana punzi yangu yaani naacha kupumu kisha napiga piga kama tunavyobembeleza watoto wadogo eneo ambalo kuna kichomi na hutoweka gafla.
 

TATIZO LA KICHOMI NI MOJA YA DALILI ZA UGONJWA MOYO

Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya.

Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi chunguza zaidi.

Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.
  1. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi
  2. Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic
Jambo la kuangalia ni je?
  1. Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?
  2. Umeinama au umelala
  3. Ukishakula chakula
Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.

Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa

wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimengenyui sawasawa linachoka.

Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan

usiweke pilipili katika kila mlo.

Tatizo jingine ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana. Chumvi inakorofisha pia

mzunguko wa damu mwilini.

Hasa kama hunywi maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…