Dawa ya Kupunguza Hasira

Mhafidhina

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2008
Posts
549
Reaction score
23
Wanajamii habari za masiku?

Naomba mnisaidie hili tatizo ili niweze kumnusuru ndugu yangu.

Nina ndugu yangu ambae yeye ana hasira sana. Pia ni mtu ambaye huwa ni negative thinker, yaani endapo utamuomba ushauri yeye huwa anawazia negatively tu. Hivi karibuni alifanya vurugu na kupigana na watu matokeo yake aliumizwa sana. Huwa anajutia sana hizo hasira zake lakini anashindwa kuzi control.

Naomba mnishauri namna ya kuweza kumsaidia huyu ndugu yangu ili aondokane na hali hii.

 
Nikutanishe nae tutafute dawa maana mie nina hasira kama zake kidogo tu nishakuja juu.
Hata sijui dawa yake nini mwenzenu labda leo tutapata dawa humu maana hali ni tete.
 
Mwambie hawe anasoma bible kuna mafundisho kibao juu ya Hasira ..
 
Anapata hasira akifanywa nini? Akibishiwa, akidanganywa au akitaniwa?
 
zako zilianza kupungua ila toka ujifiche ndo zimerudi!njoo kwa kanseling na maombi!nilikumissssss

Si kila aendaye hospitali kama Mirembe ni kichaa, you know due to hard ships in life discourse, our minds tend to adopt some madness, hivyo ni vyema baada ya kumwomba Mungu pia kuwapitia wataalamu wa mishipa na ufahamu kwa councelling na tiba.
 
Dawa yake rahisi sana. Ni mkono na sabuni tu (afu aitumie hiyo dawa akiwa amejificha)!!!!!!
 

Ajiunge na kozi ya KARATE au KUNG FU kwa sababu zifuatazo. Kwanza itamsaidia hatakuwa akipigwa kizembe na kuumizwa mara anapokasirika. Pili ili kwenye hii michezo ya marshal arts kuna syllabus ya jinsi ya kudhibiti hasira yako hasa unapochokozwa na watu.
 
Mh hii dawa akipatikana, nitaiomba nina rafiki yangu mh dakika noja nyingi ukibadilishana naye tu sentensi mbili unaye!

Kila siku anaomba mungu ampunguzie hiyo hasira nadhani akipata na dawa mambo yatakuwa swafi sana
 
Si kila aendaye hospitali kama Mirembe ni kichaa, you know due to hard ships in life discourse, our minds tend to adopt some madness, hivyo ni vyema baada ya kumwomba Mungu pia kuwapitia wataalamu wa mishipa na ufahamu kwa councelling na tiba.

Pia ajaribu kuangalia family history,si unajua nazi haianguki mbali na mti,anaweza kupata pakuanzia.
 
Mkuu hasira za kupitiliza mara nyingi huletwa na sababu fulani, most of cases huwa ni faistration za kimaisha, mara nyingi watu ambao walikua na matarajio fulani na ikawa hawajafikia malengo yao kwa kiwango kikubwa huwa wanakuwa na hisia kali na kuona kila kitu kipo against na wao, ingawa hii si kwa wote.

Hakuna dawa as labda kidonge utameza ili kumaliza hilo tatizo, huyo anahitaji ushauri nasaha wa kisaikolojia toka kwa wataalamu muhimbili
 
Dawaa kubwaa ni kunywaa glass ya majiii pindi apandwapo na asiraaa.
 
Mshauri awe anakoga au kujimwagia maji kila anapopatwa na hasira.
 
Mkuu ktk hasira mwambie asitende chochote. Kila mtu ana hasira ila cha muhimu ni kutotenda bila maamuzi ya kina. Pia mshauri aone kuwa kila kitu kinawezekana. Mfano,mtu akitukanwa anakuja juu,ila kama angejua tusi lolote lifikiriwe kubeba ujumbe wa kawaida japo unauma.

Hasira hupungka ukichukulia vitu kwa uzito tofauti.
 

Ana mwili nyumba? :roll:
 
Kuna chanzo cha yeye kuwa na hasira ovyo,yapaswa kijulikane.....wengine huona wanadharauliwa yaani ana lo self esteem,hajiamini matokeo yaka kila kitu anahasira tu.....ni katika hali gani/mazingira gani hupata hasira,ya ubishi?:coffee:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…