Endelea na endeleeni tu Kujidanganya kutaka kujifanya mnataka kushindana na Vipimo vyake Mwenyezi Mungu alivyompa kila Mwanaume aliyemuumba. Hizi juhudi zenu na hamu ya kila uchao tu kuja humu na Kuulizia jambo hilo hilo la mara sijui Ukubwa wa Uume au Nguvu za Kiume mngezihamishia katika Kuuliza ni wapi Fursa za Kiuchumi na Kiujasiriamali zinapatikana au tufanyeje ili Vijana tuondoke na Umasikini huu au tufanyeje ili tuiinue nchi yetu Kiuchumi bila shaka leo Tanzania ingekuwa inazitafuta Dubai, Singapore na Malaysia.
Watanzania tuna taabu sana / mno na tutaendelea kuwa hivi hivi hadi dunia ipinduke au mpaka Yesu Kristo wa Nazareth aje.