Dawa ya kuzuia mbao za paa kubunguliwa

Wauza mbao wezi sana hizi rangi za kuchovya eti treated wanapaka rangi za ukindu kuwaibia watu na sio dawa halisi.
Bora upake zako oil chafu.
Mimi juzi nusu nishuke na ceiling board zote zimeliwa nilipanda juu kukagua umeme
 
Mbao halisi nenda Sao hill wenyewe ila Bei SI ya kitoto
 
Dawa ya mbao ni oil chafu kama wengine wakivyosema.
Zile mbao ambazo unaona zina kama rangi ya kijani ile sio dawa.
Zile zinawekwa rangi ya ukindu.
Wafanyabiashara wengi hutumia mbinu hii ya kuloweka mbao kwenye rangi za ukindu ili wapate faida zaidi.
 
Dawa ya kutreat mbao ni gharama sana.
Laiti wangekuwa wanalaza mbao ndani ya dawa ubao mmoja ungekuwa unauzwa zaidi ya 50,000 aiseeh
 
Mbao ni Mlingoti tu hakuna mdudu anagusa labda mchwa tu wadudu wa kizembe hawez chezea
 
Tumieni mbao za milingoti haziliwi na wadudu hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…