Dawa ya macho ilisababisha kuwekwa nyuma ya nondo ugenini msumbiji jijin nampula

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Aman iwe nanyi wapendwa katika bwana

Kama kichwa cha habar kinavyosomeka hapo juu


Ilikuwa ni mwaka juz pale nilipo amua kutoka jimbo la caboligado na kuelekea beira mwisho wa siku niweze kufika maputo

Nilianza safar stand kuu pemba, nikipanda bas la maning nice kuelekea jijin nampula ili kesho yake niunge had jijin beira, kabla sijafika nampula mjin tulikuta belia kubwa sana yenye get mpakan mwa nampula na caboligado, gali ilipigwa mkono tukasimamisha, maafisa wa jeshi la polici maarufu kama policia waliingia ndan ya bus na kuanza kuomba paspot maarufu kama docomento


Wagen tulikutwa wengi wachina wawili, wanaigeria watatu na wasomali saba. Wenzangu hawakuwa na pasport lakin mimi nilikutwa na dawa ya macho kitu kilichozua utata,hofu na tafran kubwa sana kwa maafisa wa police
Niliwekwa chin ya ulinz mkali huku nikinyoshewa silaha kali za kivita kama SMG NA AKA 47, wenyewe walidai kuwa ile dawa ya macho ni madawa ya kulevya niliwaelimisha sana kuwa hii ni dawa ya macho na mimi ni mgongwa hivyo bas huwa natembea nayo popote pale. Lugha ya kizungu maana wao lugha yao ni kireno ilikuwa ni ngumu sana hivyo nilitumia kiswahili lakin napo pia ilishindikana kuelewana ilibidi niwatukane matus ya kisukuma hawakujua namanisha kitu gan


Wenzagu wale waliwekwa lupango ambayo ni tofaut na mimi niliyewekwa lupango chin ya uangaliz mkali nisije nikatoroka nikawaacha, nilikaa nyuma ya nondo kwa mda wa siku tatu had maafisa kutoka juu walipofanya uchunguz na kugundua kuwa ile ni dawa ya macho na wala si madawa ya kulevya


Niliteseka sana aisee nilikuwa nafunga na kusali, niliachiwa nikaendelea na safari yangu ya kwenda beira hati maye nikafika maputo nikiwa salama japo nilitaabika sana njian

Nilipita NAMPULA, ZAMBEZ, KILIMAN baada ya kufika kiliman nilinyoka kwenda jiji la TETE kwa ndugu kidogo na kesho yake nikaendela na safar had beira


LONDON BABY
 
Ningekuwa mimi nisingeichukua...maana hawachelewi kukukamata tena sehemu nyingine
Niliona tu nichukue maana macho huwa yananisumbua sana na kule dawa kama ile nisinge pata
 
Ulishindwa nini kuwaaminisha kwa kujiwekea machoni ili waone kama ni dawa macho kweli?

Hiyo dawa ilikuwa ya matone au ya kupaka kama mafuta?


Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…