Elections 2010 Dawa ya makundi ndani ya CCM, ni Upatanishi au Hongo ? Nani amfunge paka kengele ?

Elections 2010 Dawa ya makundi ndani ya CCM, ni Upatanishi au Hongo ? Nani amfunge paka kengele ?

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592
Kikundi cha kigaidi cha Mafia kina njia moja ya kunyamazisha upinzani wowote ule uwe wa ndani au wa nje kwa kutoa kinachojulikana kama an offer one cannot refuse ! Kwa tafsiri nyepesi ni kuwa ukikubaliana na masharti wanayokupa utanufaika na kubaki salama lakini ukikataa umejimaliza na hutakuwa salama wewe pamoja na familia yako.

Hivi sasa tunasikia ndani ya CCM wako watu watatu wanazunguka wakipatanisha makundi ndani ya CCM kwa kuwapa masharti wahusika - offers they cannot refuse. Watu hao ni mgombea Uraisi kupitia CCM Jakaya Mrisho Kikwete, Mkewe Mama Salma Kikwete na mwanaye Ridhwani Kikwete.

Kwa bahati mbaya hawa watu wana nguvu kubwa kwani hakuna wa kuwahoji hata kama matendo yao yanatia shaka, ni nje ya taratibu ama yanapingana na sheria. Si Hosea wa TAKUKURU, Tendwa wa Usajili wala Makame wa NEC ana ubavu wa kuwahoji kwa vitendo vyao wakati huu tunapoelekea Uchaguzi Mkuu.

Matendo haya yanafanyika waziwazi na sheria zinavunjwa tukishuhudia kwa macho yetu lakini vinafumbiwa macho na mamlaka zote husika kwa sababu tu wahusika ni CCM. Je hali hii inaashiria nini kama wanaofanya hivi tutawapa tena miaka mitano ya kuendeleza huu UMAFIA - hapana mwaka huu lazima uwe wa ukombozi !
 
Back
Top Bottom