Dawa aina ya Lumerax 80/480 mikoa ya Kaskazini ilikuwa inauzwa sh 5,000 haijapita miezi 5 toka ninunue dawa hiyo ili inisaidie kutibu malaria, leo hii nimeenda karibia maduka yote ya dawa nimeambiwa inauzwa sh 10,000, najiuliza kwanini dawa hii imepandishwa bei namna hii, kama mtu mwenye uwezo mdogo hawezi kumudu gharama hii serikali itamsaidiaje, hii ni dawa yenye uwezo mkubwa sana kutibu malaria.
Miaka ya nyuma serikali ilitoa ruzuku kwa dawa za malaria ili wananchi watibiwe kwa unafuu leo hii imekuwa ni dawa ghali sana. serikali iliangalie sana hili
Miaka ya nyuma serikali ilitoa ruzuku kwa dawa za malaria ili wananchi watibiwe kwa unafuu leo hii imekuwa ni dawa ghali sana. serikali iliangalie sana hili