Habari Wanajamii,Tafadhalini ndugu naomba mnijurishe dawa bora ya maralia kwa mtoto chini ya mwaka mmoja,ambaye ni mara yake ya kwanza kuugua maralia,ipatikanayo hapa nchini Tanzania,Nitashukuru sana iwapo pia nitafahamishwa Hospitali yenye daktari bingwa wa watoto hapa nchini Tanzania.Asanteni sana
Wewe unaonekana hapa ni mgeni.....
Naweza jilinda vipi dhidi ya Malaria?
- Msafiri: Kama unasafiri hadi kwenye eneo linalolotambulika kwa Malaria,mtembelee daktari wako ili akupe dawa mahsusi ya kupambana na Malaria ya eneo unalotembelea.Hakikisha umefuata maelezo vizuri.
- Wenyeji wa maeneo yalioadhirika na Malaria: Mbu wa aina ya anopheles hupenda kuuma watu nyakati za macheo na machweo kwa hivyo ni bora kujikinga nyakati hizi.Wakati wa machweo unaweza keti ndani ya nyumba iliyoekewa dawa na usiku unaweza kulala neti iliyotibiwa.
- Haribu sehemu mbu wanapozaliana: Kipindi cha mwisho katika ukuaji wa mbu hufanyika majini.Mbu wa aina ya anopheles hupendelea maji yasiyo ya chumvi.Ni muhimu kuharibu ama kunyunyuzia na dawa sehemu zote ambazo mbu wanaweza kutaga mayai.Unafaa kutoa chupa,ndoo ama chochote ambacho kinaweza kusimamisha maji,bacillus thuringiensis(Bti) dawa asili ya kuua wadudu kutoka BioVision inaweza kutumiwa kuua mbu wachanga bila kuharibu maji.
- Watoto na mama waja wazito lazima wakingwe na Malaria: Nchini Kenya,wanawake waja wazito wana haki ya kupata matibabu 2 ya bure na neti zilizotibiwa. Chukua moja kutoka katiki kliniki yako.
- Neti zilizotibiwa: Kila mtu anapaswa kupata neti iliyotibiwa.Kuna aina mbili ya neti hizi nchini Kenya ambazo zinauwa mbu pindi tu wadudu hawa wanapozigusa.Kuna zile zinazopaswa kutibiwa kila baada ya miezi 6nba PowerTabs na zile zinazodumukwa miaka 3 hadi 5 baada ya kutibiwa