Nenda MNH wana-specialists wa masikio watakupima na kugundua tatizo lako,mimi ni muathirika wa tatizo hilo ambalo kwa kitaalam linajulikana kama Tinitus,ugonjwa huu unasababishwa na kufanya kazi sehemu zenye kelele nyingi,kama una tatizo la kupiga chafya nyingi(kutokana na alergy) au wakati mwingine linatokea kutokana na umri mkubwa kwa baadhi ya watu miaka hamsini na kuendelea.Matibabu yanatokana ugonjwa umekaa nao kwa muda gani,unaweza ukapatiwa dawa na hiyo hali ikaisha,unaweza kufanyiwa operation ukapona kabisa ikishindikana utapewa vifaa vya kukusaidia kusikia vizuri.Unaweza pia ku-Google hiyo Tinitus ili upate maelezo ya kina.