Dawa ya NYONGO au Heartburn

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2008
Posts
1,518
Reaction score
24
Tafadhali nijulisheni dawa ya kuponya tatizo la NYONGO mwilini.
Je tatizo la nyongo ndilo heartburn kwa Kiingereza?
naomba msaada.
 
Heart burn ni kiungulia, hali hii inatokana na nyongo kuzidi sana tumboni, na kuna sababu zake,

kwa vile umetaka kujua heart burn na nyongo, jibu ndio hilo, sababu zake utajulishwa siku nyngine.
 
heartburn kuna magonjwa yana majina mazuri sana, unaweza kutamani uyapate.
 
Inazidi mkuu.

Kule kwetu ikikupata hii tunakunywa magadi. Yale ya kutengeneza kiburu. Kwa huku naona wengine wanakulaga majivu. Mimi nikinywa maziwa fresh huwa namaliza kabisa. Au labda kwa kuwa cha kwangu kinasababishwa na mitungi.
 
Heart burn ni kiungulia, hali hii inatokana na nyongo kuzidi sana tumboni, na kuna sababu zake,

kwa vile umetaka kujua heart burn na nyongo, jibu ndio hilo, sababu zake utajulishwa siku nyngine.

Asante mkuu,
Nitashukuru kama utanijulisha hizo sababu na tiba yake.
 
Mtoa bandiko kabla sijachangia una tatizo la kuongezeka uzito? na umewahi kucheki cholestral level yako? Je wewe ni mlaji wa nyama sana red mt au kilaji? pilipili je?
 
Kuna jamaa naona huwa anatumia magnessium tabulates kupunguza. Ila muone daktari (mimi siyo medical dk)
 
Mtoa bandiko kabla sijachangia una tatizo la kuongezeka uzito? na umewahi kucheki cholestral level yako? Je wewe ni mlaji wa nyama sana red mt au kilaji? pilipili je?

Mkuu Ngulli,
Maswali yako yanaashiria mema katika kufikia suluhisho.

1. Mwenye tatizo hili hana tatizo la kuongezeka uzito.
2. Si mtumiaji sana wa red meat ila hutumia kwa uchache.
3. Hupenda sana pilipili japo hutumia mara chache sana.
4. Hajawahi kupima colestral level.
 
Kule kwetu ikikupata hii tunakunywa magadi. Yale ya kutengeneza kiburu. Kwa huku naona wengine wanakulaga majivu. Mimi nikinywa maziwa fresh huwa namaliza kabisa. Au labda kwa kuwa cha kwangu kinasababishwa na mitungi.

Chris,
Huyu mwenye tatizo hili hata akitumia maziwa au magadi, hapati suluhisho la kudumu.
 
Tatizo la nyongo lisipozibitiwa linasababisha ulcers/vidonda vya tumbo kwa vile inakwangua ute ute pembeni mwa utumbo kwa jina la kitaalamu unaitwa mucus so kunabakia chubuko. Pia inaweza kusababisha stomach cancer.

Nyongo/bile inasabishwa na ulaji wa vitu vyenye acid kali kama pombe.
Inaweza kumwagika tumboni kwa wingi kutokana na mshituko wa hofu ya uoga wa situation yeyote ile. au hofu kwa mfano kufiwa etc.

Attachments

  • BK9780854048465_m.jpg
    7.6 KB · Views: 333

Apime pia bilurubin total & bilurubin level
 
Asante Ngulli,
Huyu mhusika si mtumiaji wa pombe na wala haimpati kwa ajili ya hofu.
Nitatzo la zaidi ya miaka kumi sasa.
Awe katika hali ngumu au raha, hali hii hujitokeza tu.
 
Tafadhali nijulisheni dawa ya kuponya tatizo la NYONGO mwilini.
Je tatizo la nyongo ndilo heartburn kwa Kiingereza?
naomba msaada.

Heartburn sio nyongo, ni kiungulia!!!! na tatizo hilo linatokana endapo mfumo wako wa usagaji chakula mwilini haufanyi kazi ipasavyo/vyema/sawia!!

"Heartburn is a painful burning sensation in your chest, caused by indigestion"
 
Endeleza hoja mkuu.
Ufumbuzi wake ni nini?
 
Asante Ngulli,
Huyu mhusika si mtumiaji wa pombe na wala haimpati kwa ajili ya hofu.
Nitatzo la zaidi ya miaka kumi sasa.
Awe katika hali ngumu au raha, hali hii hujitokeza tu.

nadhani tatizo la huyo muhusika ni kwenye suala zima la maakuli! je, anakula kwa wakati unaotakiwa? je anakula mkusanyiko wa chakula bora? anafuata kanuni za lishe? ukizingatia hayo mambo yatakuwa shwari!!

Heartburn sio nyongo, ni kiungulia!!!! na tatizo hilo linatokana endapo mfumo wako wa usagaji chakula mwilini haufanyi kazi ipasavyo/vyema/sawia!!

"Heartburn is a painful burning sensation in your chest, caused by indigestion"
 
Kama ni miaka 10 tayari ana ulcers na kama ana ulcers atibu ulcers kwanza na kutibu ulcers kunaanzia kichwani then ndio tumboni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…