- Source #1
- View Source #1
Nimeipata WhatsApp hii, Je ni kweli? Inadai kuwa ipo dawa mpya inayojulikana kama 'strawberry quick' ambayo imekuwa ikitolewa kwa kificho kwa wanafunzi kwa malengo ambayo hayajafahamika hadi sasa. Taarifa inadai zaidi kuwa Watoto wanakula wakifikiri kwamba ni peremende na wanakimbizwa hospitali wakiwa katika hali mbaya. Pia inakuja katika chokoleti, siagi ya karanga, cola, cherry, zabibu na machungwa.
JamiiCheck tusaidieni kufuatilia!
- Tunachokijua
- Kumekuwapo na ujumbe unaosambazwa kwenye makundi ya WhatsApp ukiwataka wazazi kuchukua tahadhari na kuwaelimisha watoto wao kutokubali kupokea zawadi wanazopewa na watu wasiowafahamu, na kwamba Dawa ipo dawa mpya inayotolewa kwa wanafunzi wa shuleni inayoitwa strawberry quick.
"Tafadhali wasilisha hii hata kama huna watoto shuleni. Wazazi wanapaswa kujua kuhusu dawa hii. Hii ni dawa mpya inayojulikana kama 'strawberry quick'. Kuna jambo la kutisha sana linaloendelea shuleni hivi sasa ambalo sote tunapaswa kufahamu. Kuna aina ya crystal meth inayozunguka. ambayo inaonekana kama miamba ya sitroberi (pipi ambayo inasisimka na 'kutoka' kinywani mwako). Pia inanuka kama sitroberi na inatolewa kwa watoto katika uwanja wa shule. Wanaiita strawberry meth au strawberry quick.Watoto wanakula wakifikiri kwamba ni peremende na wanakimbizwa hospitali wakiwa katika hali mbaya. Pia inakuja katika chokoleti, siagi ya karanga, cola, cherry, zabibu na machungwa. Tafadhali waelekeze watoto wako wasikubali pipi kutoka kwa wageni na hata wasikubali pipi inayoonekana kama hii kutoka kwa rafiki yako (ambaye anaweza kuwa amepewa na kuiamini ni peremende) na kupeleka chochote ambacho wanaweza kuwa nacho kwa mwalimu, mkuu wa shule, n.k. mara moja. Tuma barua pepe hii kwa watu wengi uwezavyo (hata kama hawana watoto) ili tuweze kulea. ufahamu na kwa matumaini kuzuia majanga yoyote kutokea..!!
Tafadhali sambaza Kwa Kiwango cha Juu ili kuongeza ufahamu kwani inasaidia sana" Unabainisha ujumbe huo.
Kwakuwa suala hili linahusisha afya ya umma, na kwasababu Jamii inapaswa kupata taarifa sahihi wakati wote, JamiiCheck imefuatilia undani wake na kuja na majibu yafuatayo.
Uhalisia wake
Ufuatiliaji wa kina uliofanywa na JamiiCheck umebaini madai haya si ya kweli, yamekuwepo Mtandaoni kwa miaka mingi na yamekuwa yakijirudia kwa nyakati tofauti huku baadhi ya mamlaka za nchi mbalimbali zikiyakanusha.
Ukaguzi wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno 'strawberry quick' umeonesha kuwa suala hili halipo Tanzania pekee. Ujumbe huu unaonekana kusambaa nchi nyingi duniani. Tazama hapa, hapa, hapa na hapa.
Kwa kutumia Google Reverse Image Search, kumbukumbu za picha za Mitandao zinaonesha kuwa picha inayosamba ikiambatana na madai haya imekuwepo mtandaoni kwa miaka mingi, na ilijipatia umaarufu mkubwa mwaka 2017 ambapo madai haya yalisambaa kwa kasi duniani. Aidha, madai hayo hajayabadilika, yamekuwa yakisambazwa kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine kwa lugha tofauti.
Kwa Tanzania, hadi Februari 9, 2025, hakuna taarifa rasmi juu ya uwepo wa dawa hizi.
Ni muhimu kuwa makini unapopata taarifa yoyote ile ya kushtua kwani wapotoshaji hutumia mbinu ya kuteka hisia za msomaji ili asambaze ujumbe huo kwa haraka. Pamoja na kwamba ni muhimu kuchukua tahadhari zote za kuwalinda watoto, ni lazima tukumbuke pia kuwa taarifa potoshi zinaweza kuzua taharuki na kuleta sintofahamu kubwa kwenye jamii.