PreGE2025 Dawa ya Uchaguzi Huru na Haki ni nini hasa? Nisaidieni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

tripof

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2024
Posts
853
Reaction score
1,147
Tumefika mahali wengine tumechanganyikwa na dhana ya No Reform No election, Mimi naomba wachambuzi wa mambo mnisaidie.

Ukiangalia ni kweli uchaguzi wa 2019, 2020 ulikuwa mbaya haijawahi kutokea na Serikali akiwemo Rais alikiri hivyo, lakini mwaka 2024 hali ikajirudia na hatimaye CHADEMA na ACT wamekuja na movement za mabadiliko ya katiba, Sheria na Kanuni.

Swali la msingi je hiyo itakuwa tiba ya tatizo la maovu kwenye uchaguzi? Hapa ndipo tunapaswa kufikiri zaidi ndiyo maana Wasira anaweka utetezi kuwa mabadiliko yamekwisha fanyika na yuko sahihi kwa kiwango fulani,

Mimi ninaleta hoja chokozi kuwa inawezekana kuna "attributes" zaidi ya hizo hata kama katiba na sheria zitabadilishwa. Je kanuni ya "impartiality" au "neutrality" kwa watumishi wa umma ipo, sasa kulikoni. je haitekelezeki kwa nini? hali ikoje?

Mimi ninashawishika kuamini kuwa Chadema wahoji pia mambo mengine nyemelezi kama ukosefu wa maadili na nidhamu ya wasimamizi wa uchaguzi, maelekezo kutoka juu, uzalendo, rushwa ya vyeo, mtizamo hasi na uelewa mdogo wa watendaji kuhusu dhana nzima ya uchaguzi huru na wa haki, teknolojia,umilki wa vyombo vya dola na matumizi yake yasiyo mazuri.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Hofu ya kunyanganywa madaraka nk. Haya mambo hayahitaji mabadiliko ya katiba na sheria pekee bali utashi wa kisiasa zaidi. vyote vinahitajika.Chadema wanaweza kupewa mabadiliko wanayoyataka na bado kura zikaibiwa au uchafuzi ukafanyika kama kawa,wawe makini kujua nini hasa wanatafuta. Tafakuri nzito
 
Wameshasema nini wanatafuta, unaposema wajue nini wanataka unamaanisha nini?
 
Wakitokea wabishi wachache wa kukinukisha mtaani, mbona kesho yake tu uchaguzi huru, Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi; vyote vinapatikana.

Shida iliyopo kila mtu anamnyooshea mwenzake kidole kujitokeza barabarani kukinukisha!!
Na huu woga ndiyo unaowapa jeuri watawala kuendelea kuwageuza wananchi kuwa misukule.
 
Umechanganyikiwa nini mkuu?,

Hakuna mabadiliko kwenye sheria za uchaguzi hakuna uchaguzi, Note uchaguzi hautasusiwa bali utazuiliwa ,na wajipangao watakua viongozi batili dunia hii,sasa wapi hujaelewa.

Usipende msikiliza mzee wasira ,utapoteza focus ,kaisha jichokea na tumbo lake kubwa
 
Unatafuta kupotezea watu muda tu na kuwavuruga akili. Huna lolote la maana katika kuchangia mabadiliko yanayo tafutwa.
 
Uchaguzi Mkuu upo palepale.
 
Hatimae madai ya Lisu yamekuwa madai ya chadema, ukweli jamaa ana nguvu ya uheshimiwa,
Tunakua na tabia za kitoto Bado, Yale mambo ya ukitembelea ushuani ukazoeshwa nyama unaanza kuchukia dagaa ni tabia ya kitumwa

Wakandarasi awamu hii Lisu amewatuma na no reform no election, ametuambukiza tabia ya upinzani wa kinachoendelea, Leo wajinga wanatamba Kwa kutokwenda kujiandikisha, ukweli no reform no election,

Kuna aina mbili za uheshimiwa
Unaweza kuwa mheshimiwa Kwa kuunga juhudi kinachoendelea, lakini vile vile unaweza kuwa mheshimiwa Kwa kupinga kinachoendelea, Hawa ni democrats au kizazi Cha hoja,

Choose side either no reform no election or election, no reform,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…