Dawa za asili kwa maumivu ya jino

Paka paka

Member
Joined
May 9, 2016
Posts
21
Reaction score
7
Maumivu ya jino ni moja ya maumivu mabaya sana kuyapata, maumivu mengine mabaya ni ya sikio. Jino linaweza kupatwa na mavumivu ambayo yanaweza kupelekea jino kutoboka na hata kuong’olewa kabisa. Dawa zifuatazo zinaweza kutuliza maumivu ya jino na hata kuliziba kabisa iwapo tayari limeanza kutoboka.

1. Asali yenye mdalasini

Chukua asali vijiko vidogo vitatu na uchanganye na mdalasini ya unga kijiko kimoja. Pakaa mchanganyiko huu kidogo kidogo juu ya jino linalouma kutwa mara 3.

2. Aloe vera (mshubiri)

Pata aloe vera fresh na uchane kupata maji maji yake (utomvu) na unyunyize juu ya hilo jino linalouma kidogo kidogo kutwa mara 2.

3. Mafuta ya nazi na karafuu

Chukua karafuu 3 zitwangwe kwenye kinu, changanya na mafuta ya asili ya nazi kijiko kidogo kidogo kimoja uliyotengeneza mwenyewe nyumbani. Pasha kwenye moto kama dakika tatu, ipua na usubiri mchanganyiko wako upoe. Paka mchanganyiko huu juu ya jino linalouma na uache kwa dakika 7 kisha jisukutue kinywa na maji.

Zingatia sana kutumia chumvi ya kutosha kila siku na mazoezi ya viungo

Epuka vyakula vitamu sana vya madukani, ice krimu, pipi,na soda zote na vingine vya jamii hiyo.
 
mi nachojua dawa ya jino bovu ni kulitoa tu. kwanza jino bovu linasababisha kinywa kunuka hata malovee inakuwa shida mambo ya kiss kiss
sasa uweke alocera ilivochungu mtu akikubusu huo uchungu si utakutana na thread humu jf mdomo wa mpenzi wangu mchungu unanuka.....no way
 
Sasa jino la juu utaling'oa?
 
Kwanini jino linauma

Ipi mechanism ya hizi dawa kwenye jino linalouma??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…