Dawa za Kihaya

ASHA NGEDELE

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
784
Reaction score
327
Habari zenu wakuu..

Nina mtoto wa jamaa yangu anaumwa ugonjwa wa Sickle cell na ndio kwanza ana miaka mitatu. Anahangaika sana kushindana na crisis za uvimbe na maumivu makali sana anayopata mtoto.

Huu ugonjwa hauna Tiba bali Tiba pekee ya kihospitali ni Bone Marrow/Spem Cells transplant ambayo gharama yake inazidi $20,000, haifanyiki Tanzania, lazima apatikane >95% matching donor, ina'involve Chemotherapy ambayo inaua baadhi ya cells za mwili, kuna posibility ya transplant kushindwa, ina risk ya kumletea madhaara ya mwili na pia husababisha kifo kwa mgonjwa.

Huyu bwana ana ndugu yake aliumwa huu ugonjwa zamani sana akapewa dawa na bibi wa KIHAYA na mpaka sasa anakaribia miaka 40 hajaumwa tena na anaishi maisha ya kawaida kabisa na watoto watatu. Tatizo kubwa huyo mama wa Kihaya hajui pa kumpata tena na kwa sasa dawa za Uwongo zimekua nyingi sana.

Yeyote mwenye kufahamu Daktari wa Asili kutoka hio mikoa ya Kaskazini Magharibi naomba mawasiliano yake nimpatie huyu jamaa yangu wa karibu sana. Awe Daktari mwenye rekodi ya kutibu kweli na sio longolongo.

Nitashukuru sana wandugu.

Asante.
 
Dawa za Kihaya ni nzuri sana kuna mama mmoja yupo pale getini boda ya Mtukula aliniuziaga dawa ya maleria daah ni kiboko.yani huwa ikiisha lazima niwaagize wafanyakazi wa taqwa bus ni mwaka wa 4 sasa sijawahi kumeza dawa za madukani. Ila ni kweli nao wasanii wamekuwa wengi sana jaribu kumtafuta Muhaya mtu mzima akusaidie aongee na wazee wao huko kwao
 
Wahaya wanaotibu ni wengi ila baadhi ya dawa zinaweza prove failure ila ni kuendelea kutumia bila ya kukata tamaa na MUNGU atasaidia kwa mapenzi yake
 

Asante nafikiri option ya kutafuta watu wazima ni nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…