Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Dalili za vidonda vya tumbo.
dalili zipo nyingi lakini kubwa ni kusikia maumivu kwenye mvuko wachakula na kusambaa hadi juu ya kitovu
pia kama ni vidonda vya tumbo vilivyo sababishwa na utumiaji mbaya wa dawa,mgonjwa ujisikia maumivu makali wakati ana njaa pia akinywa dawa kama Aspirine.
mara nyingi maumivu hayo uwa yanahamahama hadi mgongoni na kwenye mabega na dalili nyingine ni mgonjwa kutapika,kualisha damu na kukonda.
Tiba na ushauri.
mgonjwa anatakiwa akiona dalili hizo tulizo zitaja aende hospitali kupimwa na kutibiwa.lakini ushauri ni ukosefu wa usingizi ni maradhi makubwa katika dhama zetu hizi.kwahiyo kulala ni moja ya tiba ya mwili usingizi husaga chakula na kuondoa uvimbe katika tumbo
DAWA ZINAWEZA KUSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO-2
naendelea kuelezea jinsi dawa zinavyoweza kuleta vidonda vya tumbo. Tuwe pamoja...
Dalili za vidonda vya tumbo
Dalili zipo nyingi lakini kubwa ni kusikia maumivu kwenye mfuko wa chakula na husambaa hadi juu ya kitovu.
Pia kama ni vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na utumiaji mbaya wa dawa, mgonjwa husikia maumivu makali akiwa na njaa pia akinywa dawa kama asprine.
Mara nyingi maumivu hayo huwa yanahamahama hadi mgongoni na kwenye mabega na dalili nyingine ni mgonjwa kutapika, kuhalisha damu na kukonda.
Tiba na ushauri
Mgonjwa anatakiwa akiona dalili tulizozitaja aende hospitali kupimwa na kutibiwa. Lakini ushauri ni kwamba ukosefu wa usingizi ni maradhi makubwa katika zama zetu hizi. Kwa hiyo kulala ni moja ya tiba za mwili. Usingizi husaga chakula na huondoa uvimbe katika tumbo, udhaifu na uchovu.
Kukesha usiku kucha husababisha kutosagika kwa chakula tumboni na hudhoofisha akili na pia husababisha akili kuvurugika. Kulala huleta pumziko kamilifu la mwili na akili.
Mtu anapolala metaboliki ya mwili hufanyika polepole kiasi kwamba sehemu kubwa ya vyanzo vyake vya nishati hupatikana kwa ajili ya makuzi ya afya njema ya mwili na akili.
Sehemu ya kulala inatakiwa iwe ni tulivu na isiyo na kelele, pia iwe na hewa safi na asilia. Hewa asilia zake ni kuiwezesha akili kufanya kazi barabara, na pia huongeza hamu ya kula.
Kiwango cha wastani cha kulala kinachotakiwa hutegemeana na umri, mtoto wa umri wa miaka miwili hushauriwa kulala saa 14 hadi 16 kwa siku. Miaka minne saa 12-14 kwa siku, miaka sita hadi minane saa 11-12 kwa siku, miaka minane hadi 11 saa 10-11 kwa siku, miaka 14 hadi 18 saa 8-9 kwa siku. Watu wazima wanahitaji saa za kulala kati ya sita na nane.
DAWA ZINAWEZA KUSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO -3
katika safu hii tunajadili tatizo la vidonda vya tumbo vinavyotokana na utumiaji mbaya wa dawa mbalimbali tunazomeza. Tuliahidi kwamba kwa kumalizia mada hii tutaeleza dalili za maradhi haya na matibabu yake.
Dalili za vidonda vya tumbo
Kama tulivyosema awali kuwa vidonda vya tumbo ni ugonjwa sugu na unachukua muda mrefu kuonesha dalili lakini huwa na chanzo chake (natural history), husumbua mgonjwa kwa muda mrefu naye huhangaika kwa matibabu kwa muda mrefu na kuwa vigumu kupona kabisa japokuwa hupata nafuu pale anapokuwa anatumia dawa.
Dalili kubwa ya vidonda vya tumbo ni kuuma kwa tumbo ambako hushambulia sehemu kuu tatu au huwa na tabia kuu tatu.
Kwanza, sehemu ya tumbo inayouma huwa ni kwenye mfuko wa chakula (stomach). Maumivu huwa upande wa juu wa tumbo karibu na chembe ya moyo.
Pili, maumivu huambatana na matumizi ya chakula, wengine husikia maumivu kabla ya kula, wengine husikia maumivu baada ya kula na maumivu hujirudia mara kwa mara.
Tatu, mgonjwa kusikia maumivu ya tumbo ambayo huambatana na kutapika. Hali hii huwatokea wagonjwa ambao vidonda huziba utumbo na kumfanya aliyeathirika na tatizo hili kupoteza uzito wa mwili wake.
Lakini tukumbuke kuwa asilimia kubwa ya wagonjwa wa vidonda vya tumbo huwa hawajitambui na huwa na dalili ndogondogo kama tumbo kuunguruma , kiungulia na tumbo kujaa gesi, uswahilini wengine husema wanaumwa chemba ya moyo.
Vipimo vya kugundua vidonda vya tumbo
Zamani kulikuwa na ugumu na upatikanaji wa vipimo sahihi vya kugundua vidonda vya tumbo lakini sasa hivi ni rahisi kuutambua kwa sababu vipo vingi kama vile kupigwa picha ya x-ray kipimo hicho hujulikana kama Baliam meal.
Baada ya uchunguzi wa uhakika uliogundua kuwa wagonjwa wengi wa vidonda vya tumbo husababishwa na bakteria waitwao H pylori na kurahisisha uchunguzi ambao hufanyika kwa vipimo vya damu ambavyo hujulikana kwa majina mbalimbali.
Majina ya vipimo hivyo ni kama vile Urea breath test, Faecal anligen test, Rapid urea breath test na H pylori test. Lakini pia kuna vipimo ambavyo hufanyika kwenye hospitali kubwa na za kisasa kama Microbiological culture ( yaani gold standard).
Kuna kipimo cha kumulika utumbo kupitia mdomoni kinaitwa Endoscope, ni muhimu kwa daktari kuweza kuona jinsi vidonda vilivyo vikubwa au vidogo na kuwa rahisi kutoa tiba.
Matibabu na ushauri
Ukweli ni kwamba mgonjwa ambaye hajapata madhara (complication) hupata matibabu sahihi hususan kama ana bakteria wa H pylori kwani huweza kupona kabisa.
Vizuri wagonjwa waende hospitali kupimwa hasa wale ambao watakuwa wanaona dalili tulizoziainisha.
dalili zipo nyingi lakini kubwa ni kusikia maumivu kwenye mvuko wachakula na kusambaa hadi juu ya kitovu
pia kama ni vidonda vya tumbo vilivyo sababishwa na utumiaji mbaya wa dawa,mgonjwa ujisikia maumivu makali wakati ana njaa pia akinywa dawa kama Aspirine.
mara nyingi maumivu hayo uwa yanahamahama hadi mgongoni na kwenye mabega na dalili nyingine ni mgonjwa kutapika,kualisha damu na kukonda.
Tiba na ushauri.mgonjwa anatakiwa akiona dalili hizo tulizo zitaja aende hospitali kupimwa na kutibiwa.lakini ushauri ni ukosefu wa usingizi ni maradhi makubwa katika dhama zetu hizi.kwahiyo kulala ni moja ya tiba ya mwili usingizi husaga chakula na kuondoa uvimbe katika tumbo