Dawa zipi nzuri kati ya za wamasai na za maustadhi?

Wakuu naomba mnijuze kati ya dawa za mmasai na hizi za kisunna wanauza maustadh kwenye maduka ya madawa yao zipi zinafanya vizuri katika tiba? Nisaidieni ili niamue kwenda kwa masai ama ustadhi
Kazi ya wewe kupona ni kazi ya Allah kutumia kwako dawa ni sababu ya wewe kuweza kupona lakini mwenye sifa ya kuponya ni ALLAH lakini mpaka utumie maarifa aliyowapa binadam wenzako ndio ma dr, maustadh, wamasai na wengineo haram ni kujitibu kwa imani ya ushirikina tu. Mfano kupiga ramli kutaka kujua kwanini umeumwa nani kakuroga ,kwenda kuzika vitu makaburini ,kunywa damu za wanyama tiba hizo ndio haramu,na hata kuiamini dawa ndio imekuponya pia si vyema utakuwa umeipa sifa ambayo si yake .Hivyo kuhusu mmsai na ustadh unaweza ukatumia dawa yoyote kati ya hizo lakini isifungamane na ushirikina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…