Mkuu Kennedy,
Siku ina masaa 24, na dawa(dawa nyingi) daktari anaandika kulingana na uwepo wa masaa 24 katika siku.Hii ikiwa na maana anafanya hesabu(KULINGANA NA DOZI INAYOHITAJIKA) yaani dawa mtumiaji atumie kila baada ya masaa 24, au masaa 12, au 8 au 6...Hivyo basi hufanya hivi;
a)1x1 (Humaanisha kila baada ya masaa 24)
b)1x2 (kila baada ya masaa 12)
c)1x3 (kila baada ya masaa 8)
d)1x4 (kila baada ya masaa 6)
Sasa kwanini daktari anakuamvia kunywa mara tatu? anamaanisha alifanya hesabu katika masaa 24 ya siku, dawa aliyokupa unatakiwa kutumia kila baada ya masaa 8..yaani masaa ya siku nzima ukigawanya kwa masaa ya kutumia dawa YAANI 24/8= 3...so kwa wagonjwa wengine(NI NGUMU kuelewa au kukumbuka) so unapomueleza tumia asb, mchana na jioni ni nafuu.
KUJIBU SWALI LAKO:
Si vyema kutumia zaidi ya dozi(kumvuka kila dawa ina madhara)..hivyo unaweza kuathiriwa na madhara ya dawa, ongezeko la dawa mwilini, n.k
Sijui kama umeelewa mkuu?