DAWASA imesema, hali ya upatikanaji wa Maji ndani ya eneo lake la kihuduma Dar na Pwani ipo vizuri

DAWASA imesema, hali ya upatikanaji wa Maji ndani ya eneo lake la kihuduma Dar na Pwani ipo vizuri

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
HUDUMA YA MAJI DAR NA PWANI IPO VIZURI - DAWASA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema hali ya upatikanaji huduma ndani ya eneo lake la kihuduma katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani ipo vizur na inaendelea kuimarika kupitia vyanzo vya uzalishaji wa maji vya Ruvu Juu na Ruvu Chini.

Akiongea na Waandishi wa Habari, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire Amesema kuwa vyanzo vya uzalishaji maji katika mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini inapokea maji ya kutosha na hali ya maji katika Mtoni Ruvu iko katika hali nzuri ya uzalishaji ukiacha changamoto ndogo iliyojitokeza katika Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Juu ambayo imeshatatuliwa na uzalishaji unaendelea vizuri.

Mhandisi Bwire ameongeza kuwa kazi inayoendelea kwa sasa ni kuhakikisha Maji yanayozalishwa yanasukumwa nakusambaza kwa Wananchi.

Amebainisha kuwa kwa maeneo yaliyokuwa na changamoto ya huduma ikiwemo Kinyerezi, Makabe, Mshikamano na Machimbo kazi ya usambazaji maji kwa sasa inaendelea vizuri na huduma inaendelea kuimarika.

"Mamlaka inaendelea na taratibu za manunuzi ya Pampu mpya 12 za kufunga kwenye Mitambo ya uzalishaji maji ili kuboresha na kuongeza kiwango cha uzalishaji maji ili kuhudumia wananchi wengi zaidi," amesema Mhandisi Bwire.
 
Yaani baadhi ya maeneo ya Dar maji yanatoka kwa mwezi mara moja na yakitoka ni maji chumvi kabisa hayanyweki wala kutumika kwenye baadhi ya matumizi muhimu.

Kwasasa eneo nililopo ni zaidi ya mwezi yanatoka maji chumvi tupu.

Hadi tunajiuliza Dawasa wameachana na biashara ya kuuza maji baridi na kuhamia maji chumvi?

Yaani maji yanayotoka ya Dawasa yana chumvi kuliko maji ya visima ya mtaani.
 
Tatizo la viongozi wengi huwa wanashinda maofisini wakisubiri kuletewa taarifa na wafanyakazi walio chini yao hivyo kuishia kulishwa taarifa ambazo sio sahihi na yeye kuzitoa kwa umma kama zilivyo pasipo kujiridhisha.

Mfano kitu alichokiongea hakina ukweli maana kiuhalisia maji yamekuwa adimu sana na yakitoka basi ni mji chumvi.
 
Back
Top Bottom