The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira DAWASA inatekeleza ujenzi wa vituo nane(8) vya kisasa vya kuchakata majitaka/takatope vyenye thamani ya Bilioni 16 katika jiji la Dar Es Salaam ambavyo itasaidia kupunguza gharama za kuzoa majitaka kutokana na ufinyu wa maeneo ya kuyahifadhi.
Akizungumza baada ya ziara ya kuwaonyesha Wenyeviti wa mitaa kutoka Wilaya ya Temeke miradi ya DAWASA iliyopo wilayani humo Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji na Usambazaji Maji, Mhandisi Tyson Mkindi amesema lengo la ziara hiyo ni kuwaonyesha jitihada za serikali katika kuboresha huduma za afya ili waweze kuwaelewesha wananchi wao kwa sababu wao wapo karibu nao zaidi.
Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa leo Wenyeviti hao walitembelea kituo cha kuchakata takatope cha Vikunai, kituo cha kuzalisha na kusambaza maji cha Mtoni Mtongani, na kisima cha maji cha Yombo.
Mhandisi Mkindi ameeleza kuwa miradi hiyo 8 ikikamilika itakuwa na faida nyingi ndani yake ikiwemo kupatikana kwa mbolea, maji safi ya kuweza kutumika kwa shughuli za kibinadamu, ajira za kudumu, pamoja na uzalishaji wa miche ya miti katika kila kituo ambayo itasambazwa katika wilaya zilizopo Dar Es Salaam.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa mitaa ya Temeke Sharifu Mustafa Jumbe ameishukuru DAWASA kwa kuwajuza juu ya miradi hiyo na kueleza kuwa uelewa waliopata utawasaidia kwenda kuelimisha wananchi juu ya huduma ambazo DAWASA inatoa.
Naye Sara Shomari Mwenyekiti wa mtaa wa Jeshi la Wokovu pamoja na Yonathan Landa Mwenyekiti wa mtaa wa KekoMachungwa wamesema mradi wa Vikunai utawasaidia wananchi wake kupunguza gharama ambazo wao hulipa ili kupata huduma ya kunyonya takatope pamoja na kusaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana.
DAWASA inatekeleza mpango wa kukutana na Wenyeviti wa mitaa katika wilaya zote za jiji la Dar Es Salaam kwa ajili ya kutembelea miradi iliyopo katika wilaya zao pamoja na kuwapa semina lengo likiwa kujenga mahusiano ya karibu na wenyeviti hao pamoja na kuwapa elimu juu ya huduma ambazo mamlaka hiyo inatoa.