Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Wiki mbili zilizopita kulitokea changamoto ya bomba la maji kupasuka maeneo ya Maili Moja – Kibaha, hali hiyo ikasababisha maeneo mengi kukosa maji, tuliporipoti DAWASA – Kibaha kila siku wakawa wanatuambia wanarekebisha lakini bado huduma hazijarejea.
Hali hiyo inatupa changamoto kubwa Wakazi wa Maili Moja hasa maeneo ya Muheza na jirani, kuna watu wanauza maji kwenye magari kiasi kwamba tunajiuliza au kuna mchezo kati ya mamlaka na wanaofanya biashara hiyo?
Pia soma ~ DAWASA: Huduma ya Maji Muheza Maili Moja itarejea, mabomba yaliyoharibika yametengenezwa