Dawasa Kinyerezi naona mnakula kwa urefu wa Kamba

Dawasa Kinyerezi naona mnakula kwa urefu wa Kamba

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Salaam!

Salaam toka Kinyerezi mtaa wa Sadani kwa Babu Ali,huu mtaa una miezi miwili hauna maji,ratiba ya kufungulia maji mara moja kwa mwezi mtaa huu inarukwa either kwa makusudi au wanatuona sisi manyani,kuna mitaa michache inapata maji kwa mwezi hata mara 3 kimpango mkakati ili itumike kama ngao na kuaminisha wakubwa majibu yao kuwa Kinyerezi maji yapo ila ukweli Mimi nipo hapa mtaa wa Sadani kwa Babu Ali huu ni mwezi wa pili maji hayajatoka.

Kwa sasa ili uweze kuagiza maji kwenye gari unatakiwa uwe na Shilingi 45,000. Na Kwa siku gari moja linaweza sambaza Maji kwa familia/kaya 30.

Kwa hesabu za haraka kwa siku moja gari moja linakusanya kiasi cha 1,350,000.

Bill yangu ya mwisho ilikuwa 13,000 ila mtandao mkubwa wa kuuza maji kwa njia ya magari Kinyerezi unafanya biashara kubwa,kwa hesabu za haraka kwa Siku 10 tu wanauhakika ya kuingiza 70,000,000..huku bill za maji za serikali zikiwa chini ya millioni 10.

Mtandao huu wa kuuza maji kwa njia ya magari huku Kinyerezi ni mkubwa na umeota mizizi pamoja na malalamiko ya wanachi kwa Dawasa Kinyerezi hakuna hatua zinazochukuliwa kuuwajibisha mtandao huu.

Wito kwa mamlaka nyingine za serikali kuingia Dawasa kinyerezi ili kuokoa mapato ya serikali yanayopotea,Dawasa Dar es salaam wanatakiwa kuondoa watumishi ya Dawasa kinyerezi ili kulinda heshima yao na Wizara ya Maji.
 
Kweli mkuu unachosema sijui tunaelekea wapi kama nchi kwakweli mambo ya ajabu sana,Nimekuja kumtembelea jamaa yangu juzihapa kinyerezi mwisho leo siku ya tatu maji hayajatoka nimejiuliza hii ni nini
 
Muoneni makonda

Mtumieni hata message


Halafu huyo bonnet malaya anaupigie wapi upuuz wake
 
Yani biashara ya mtu mmoja inatesa watu kila kona nchi hii ya ajabu sana
 
Back
Top Bottom