Wananchi wa mtaa wa Nyeburu uliopo kata ya Buyuni ILALA, Dar es salaam wameilalamikia mamlaka ya maji safi na mazingira DAWASA Kisarawe kwa kushindwa kufikisha huduma ya maji kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema licha ya mamlaka hiyo kushindwa kufikisha huduma ya maji kwa zaidi ya miaka miwili lakini bado wananchi wanaendelea kupatiwa ankara kwaajili ya kulipia huduma hiyo.
Akiwa katika kikao cha kujadili kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Nyeburu mwenyekiti wa mtaa huo SADATH RWETABURA akawaomba wananchi kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho wataalamu wanaipatia ufumbuzi kero hiyo.
Kufuatia malalamiko hayo Mwakilishi wa meneja wa DAWASA Kisarawe Mhandisi ERASTO MWAKILULELE akatolea ufafanuzi na namna ambavyo wamejipanga kuhakikisha mamlaka hiyo inarejesha huduma hiyo hivi karibuni.
Baadae utasikia mama mama mama mama,yaan Pwani kuna mto Ruvu,mto Rufiji ni mito mikubwa tu,kams hiyo haitoshi serikali ingeweza kutengeneza lambo kubwa kama Mindu Morogoro lets say kila mkoa lakini 2025 hii watu bado wanalia shida ya maji tunashindwa hadi na nchi za majangwa kama Qatar na UAE.
Mtu yeyote anayefanikisha Ccm kuingia madarakan either kwa kupiga kura au kwa vyovyote vile akili yake inatakiwa ipimwe