DAWASA: Kuendelea kwa matengenezo ya umeme katika mitambo ya maji ya Ruvu juu na Ruvu chini

DAWASA: Kuendelea kwa matengenezo ya umeme katika mitambo ya maji ya Ruvu juu na Ruvu chini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
TAARIFA KWA UMMA

KUENDELEA KWA MATENGENEZO YA UMEME KATIKA MITAMBO YA RUVU JUU NA RUVU CHINI

23.6.2024

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wa Dar es salaam na Pwani wanaohudumiwa na Mitambo ya kuzalisha maji Ruvu Juu na Ruvu Chini kuwa, kumekuwa na matengenezo ya umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika mitambo ya uzalishaji Maji Ruvu Juu na Ruvu Chini tangu siku ya Jumamosi Juni 22, 2024 hivyo kupelekea ukosefu wa huduma ya maji.

Pindi matengenezo yatakapokamilika , DAWASA itaendelea na uzalishaji maji na kuhakikisha huduma inarejea kwa Wananchi.

Maeneo yanayoathirika ni;
Ruvu darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Pichandege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi inn, Mbezi, Mshikamano, Msakuzi, Makabe, Kwembe Kimara,Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Segerea Msigani, Maramba mawili, Tabata, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti,Ubungo, Makuburi, Kisarawe, Ukonga, Madafu, Pugu, Uwanja wa ndege, Majumba sita, Machimbo, Kiwalani Vingunguti, na Gongo la Mboto, Kisarawe, Chamazi, Mbande, Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Madale, Goba, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu UDSM, Mwenge, Chuo Kikuu Ardhi, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Jiji.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja

0800110064 (bure) au
0735 202 121(WhatsApp tu)

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano

==

Pia soma: DAWASA mna nini na wakazi wa Mbezi Beach? Hatuna maji siku ya 3 sasa
 
Maji vipi maeneo yenu wanajamii leo?
Dah! toka asubuhi hatuna maji mpaka napoandika muda huu still nothing katika taps maeneo yetu ya Boko Basihaya, what’s going on DAWASA?
 
Hamna maji wala Dawasa hawatoi taarifa yoyote
 
Back
Top Bottom