DAWASA kuzima Mtambo Ruvu Chini kwa saa 36 Januari 30, 2023

DAWASA kuzima Mtambo Ruvu Chini kwa saa 36 Januari 30, 2023

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira Dar es Salaam, (DAWASA) imetangaza kuzimwa kwa mtambo wa kuzalisha Maji Ruvu Chini uliopo Wilayani Bagamoyo kwa saa 36 Jumatatu 30 Januari 2023

Kwa mujibu wa DAWASA, lengo la uzimaji huo ni kusafisha mifumo yote ya Mtambo ikiwemo Machujo, Matanki yote ya Maji na Mabomba Makuu yote yanayosafirisha Maji kutoka katika mtambo huo.

Kutokana na kazi hiyo, maeneo yanayohudumiwa na mtambo huo yatakosa huduma ya Maji kuanzia Jumatatu hadi Jumanne jioni.

Maeneo yatakayoathirika ni Bagamoyo, Mapinga, Zinga, Kerege, Mabwepande, Bunju, Kunduchi, Mbezi Beach, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu UDSM, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaki, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Uwanja wa Ndege, Kiwalani Buguruni, Vingunguti, Ilala na katikati ya Jiji.

1674995189832.png
 
Back
Top Bottom