KERO DAWASA Mbezi Beach mnatuona manyani tu, Aweso pita na huku tafadhali kuna shida pahala inahitaji kunyooshwa

KERO DAWASA Mbezi Beach mnatuona manyani tu, Aweso pita na huku tafadhali kuna shida pahala inahitaji kunyooshwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
593
Reaction score
1,376
Wakuu,

Nishachoka kuja kulalamikia maji hapa, mnatufanya kama watoto tunapewa pipi tumun'unye halafu mnatupokonya. Yaani kama vile sasa hivi tupo kwenye mgao, na maji bado yana harufu mbaya, ukiwatafuta majibu ni yale yale, maji yameruhusiwa yatatoka!

Ahhh Wizara ya Maji embu pitia huko nyuma uone nna post ngapi za kulalamikia maji Mbezi Beach, mnatuona manyani sana, na cha kushangaza bili iko pale pale! Wakuu mkiona mtu kaandamana hadi ofisi za DAWASA Kawe mjue itakuwa mimi, nimechoka!
 
Pengine unaemuita ndio tatizo
Anyway mwenyekiti atapita kwa kishindo.
 
Back
Top Bottom