KERO DAWASA mnazingua, mimi si wa kuamka usiku kukinga maji ya mvua ya matumizi ya nyumbani

KERO DAWASA mnazingua, mimi si wa kuamka usiku kukinga maji ya mvua ya matumizi ya nyumbani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Sijui hii mamlaka inakwama wapi, ni wiki ya nne sasa Tabata Bonyokwa hatuna maji. Hii imekuwa kero ya miaka na mikaka na bado hatujapewa ufumbuzi. Tulipangwa kuwa kinajengwa kituo cha kusukuma maji, kingekuwa tayari Aprili lakini leo hii tunaelekea Julai hakuna matumaini.

Kuna siku mabomba yanatoa upepo tu na bili inasoma, tukiwaambia kuwa mnatugawia upepo badala ya maji mnakuwa wakali, wapuuzi sana ninyi.

Leo mimi na familia tumeamka usiku wa manane kukinga maji ya mvua, si haki kabisa. Mbunge wetu Bonnah Kamori jirani yangu kabisa Bonyokwa hana habari kabisa na sisi maana kwake yamemnyookea.

Ishukuriwe sana mvua imetuokoa na kutusitiri kutoka kwenye mateso ya Serikali.

Pia soma
 
Sisi Dawasa kwa mwaka huu maji yametoka mara 2, Januari ile siku mvua kubwa ilinyesha ikaenda na nyumba Tegeta hadi watu wakaokota magari na Aprili. Baada ya hapo maji hatujawahi kuyaona.

Dar watu tunaishi kama tuko namtumbo.

Ccm hakuna kitu wataweza kufanya nchi hii kikawa reliable, miaka 60+ ya uhuru.
 
Poleni wakazi wa Dar najua sio Dar yote ni kwa wale mnaoishi maeneo ya pembezoni...
 
Sema mitaa mengine miyeyusho sana, picha linaanza kila nyumba unakuta ina matank makubwa makubwa. Ila kuna mitaa matank hamna na maji yanatoka 24/7, hii Dsm ina matabaka sana!
 
Asante serikali ya jamuhuri kufanikisha mvua wakati wa kiangazi....😡
 
Back
Top Bottom