DAWASA: Mradi wa Maji unaogharimu Bilioni 34.5 kumaliza Tatizo la Maji Ukonga, Ubungo, Kibamba, Segerea na Ilala Mwaka huu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Dar es Salaam

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire amezungumza na Wahariri na Waandishi wa vyombo vya habari Nchini leo tarehe 07 Agosti 2024 kuhusu hali ya upatikanaji wa majisafi na usafi wa Mazingira sambamba na kueleza mipango iliyopo ya kuboresha huduma ya maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na maeneo ya pembezoni.

Mkutano huu umeratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC)

BWAWA LA KIDUNDA

IMG-20240807-WA0028.jpg

Mhandisi Mkama Bwire, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA.

"Tunaishukuru Serikali ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuchukua hatua madhubuti ya kukabiliana na changamoto ya maji kwenye maeneo ya Dar es Salaam na Pwani kupitia ujenzi wa Bwawa kubwa la Kidunda litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita Bilioni 190 ya kutumika wakati wa kiangazi ili kuepusha wananchi kukosa maji, mradi unagharimu Bilioni 336 na utakamilika mwaka 2026," Mhandisi Mkama Bwire Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA.

MRADI WA MAJI DAR ES SALAAM YA KUSINI

IMG-20240807-WA0033.jpg

Bi. Everlasting Lyaro. Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano DAWASA

"Kwa sasa tunaendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa kusambaza maji maeneo ya Dar es Salaam ya Kusini ambao unalenga kunufaisha majimbo matano ya uchaguzi ikiwemo Ukonga, Ubungo, Kibamba, Segerea na Ilala ambapo mradi unajenga tenki kubwa la lita milioni 6 na unagharimu Bilioni 34.5, mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu," Mhandisi Mkama Bwire Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA.

UPOTEVU WA MAJI

IMG-20240807-WA0023.jpg

"Kuhusu suala la upotevu wa maji kwa wateja, Mamlaka imeanza na inaendelea na zoezi la kufunga mita kubwa (Bulk meters) kwa lengo la kupima kiasi cha maji kinachozalishwa na kinachotumika ili kubaini kiasi cha maji yanayopotea mitaani na kukidhibiti kwa lengo la kuboresha huduma, zoezi limeanza Kinondoni na linaendelea eneo la Kawe na Tabata," Mhandisi Mkama Bwire Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA.

MRADI WA MAJI BANGULO

IMG-20240807-WA0026.jpg

"Kwa sasa tuna endelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa kusambaza maji maeneo ya Dar es Salaam ya Kusini ambao unalenga kunufaisha majimbo matano ya uchaguzi ikiwemo Ukonga, Ubungo, Kibamba, Segerea na Ilala ambapo mradi unajenga tenki kubwa la lita milioni 6 na unagharimu Bilioni 34.5, mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu," Mhandisi Mkama Bwire Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA.

Pia soma:

1. KERO - Wakazi wa Tegeta Azania (Kwenye Nyaya za Umeme wa Zanzibar) hatuna Maji kwa Muda Sasa, DAWASA shida ni nini?

2. KERO - DAWASA mna nini na wakazi wa Mbezi Beach? Hatuna maji siku ya 3 sasa

3. KERO - Kinyerezi kuna shida kubwa ya maji, group la DAWASA WhatsApp halifanyi chochote kutatua kero hii

4. KERO - Maji Malamba Mawili ni mgao mkali, baadhi ya Wakazi walio kwenye miinuko wana miezi hawapati maji kutokana na kasi ndogo ya maji. DAWASA wafafanua

5. KERO - Maji ya DAWASA yana harufu na ladha ya Dawa kali sana, ni salama kweli?

6. Mnyika: DAWASA mnataka tufanye maandamano ya Maji DSM ndio mtoe majibu?

7. Dar: Maeneo ya Segerea hadi Kinyerezi hakuna Maji
 
Dar es Salaam

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire amezungumza na Wahariri na Waandishi wa vyombo vya habari Nchini leo tarehe 07 Agosti 2024 kuhusu hali ya upatikanaji wa majisafi na usafi wa Mazingira sambamba na kueleza mipango iliyopo ya kuboresha huduma ya maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na maeneo ya pembezoni.

Mkutano huu umeratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC)

BWAWA LA KIDUNDA

View attachment 3063811
Mhandisi Mkama Bwire, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA.

"Tunaishukuru Serikali ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuchukua hatua madhubuti ya kukabiliana na changamoto ya maji kwenye maeneo ya Dar es Salaam na Pwani kupitia ujenzi wa Bwawa kubwa la Kidunda litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita Bilioni 190 ya kutumika wakati wa kiangazi ili kuepusha wananchi kukosa maji, mradi unagharimu Bilioni 336 na utakamilika mwaka 2026," Mhandisi Mkama Bwire Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA.

MRADI WA MAJI DAR ES SALAAM YA KUSINI

View attachment 3063810
Bi. Everlasting Lyaro. Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano DAWASA

"Kwa sasa tunaendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa kusambaza maji maeneo ya Dar es Salaam ya Kusini ambao unalenga kunufaisha majimbo matano ya uchaguzi ikiwemo Ukonga, Ubungo, Kibamba, Segerea na Ilala ambapo mradi unajenga tenki kubwa la lita milioni 6 na unagharimu Bilioni 34.5, mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu," Mhandisi Mkama Bwire Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA.

UPOTEVU WA MAJI

"Kuhusu suala la upotevu wa maji kwa wateja, Mamlaka imeanza na inaendelea na zoezi la kufunga mita kubwa (Bulk meters) kwa lengo la kupima kiasi cha maji kinachozalishwa na kinachotumika ili kubaini kiasi cha maji yanayopotea mitaani na kukidhibiti kwa lengo la kuboresha huduma, zoezi limeanza Kinondoni na linaendelea eneo la Kawe na Tabata," Mhandisi Mkama Bwire Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA.

MRADI WA MAJI BANGULO

"Kwa sasa tuna endelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa kusambaza maji maeneo ya Dar es Salaam ya Kusini ambao unalenga kunufaisha majimbo matano ya uchaguzi ikiwemo Ukonga, Ubungo, Kibamba, Segerea na Ilala ambapo mradi unajenga tenki kubwa la lita milioni 6 na unagharimu Bilioni 34.5, mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu," Mhandisi Mkama Bwire Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA.

Pia soma:

1. KERO - Wakazi wa Tegeta Azania (Kwenye Nyaya za Umeme wa Zanzibar) hatuna Maji kwa Muda Sasa, DAWASA shida ni nini?

2. KERO - DAWASA mna nini na wakazi wa Mbezi Beach? Hatuna maji siku ya 3 sasa

3. KERO - Kinyerezi kuna shida kubwa ya maji, group la DAWASA WhatsApp halifanyi chochote kutatua kero hii

4. KERO - Maji Malamba Mawili ni mgao mkali, baadhi ya Wakazi walio kwenye miinuko wana miezi hawapati maji kutokana na kasi ndogo ya maji. DAWASA wafafanua

5. KERO - Maji ya DAWASA yana harufu na ladha ya Dawa kali sana, ni salama kweli?

6. Mnyika: DAWASA mnataka tufanye maandamano ya Maji DSM ndio mtoe majibu?

7. Dar: Maeneo ya Segerea hadi Kinyerezi hakuna Maji
Mvua yote ile iliyonyesha maji yameishia baharini! Tunachoweza ni kuzulura na misafara ya magari yanayokimbizana kama wendawazimu.
 
Upuuzi na kichefuchefu kabisa.kila siku story za Samia katoa fedha Kwa ajili ya bwawa la kidunda lakini matokeo sifuri.Miaka 63ya uhuru wananchi wa wilaya ya ubungo hawajawahi kuona maji ya dawasa
 
Back
Top Bottom