DAWASA ni moja kati ya idara za serikali zilizofeli sana jijini Dar es salaam, viongozi wawajibishwe

DAWASA ni moja kati ya idara za serikali zilizofeli sana jijini Dar es salaam, viongozi wawajibishwe

Hyrax

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2023
Posts
964
Reaction score
2,675
Nashindwa kuelewa sijui hawa watenda kazi wa hii DAWASA kuanzia viongozi hadi watenda kazi wa chini mmeshindwa kabisa kupata njia mbadala ya kuondoa hizi changamoto za huduma ya maji jijini dar es salaam? Jiji lenye zaidi ya watu milioni 8 Ni aibu sana kuona huduma ya maji ikisuasua nyie maangineer huwa mnafanya nini huko maofisini?!

Yaani DAWASA mmeshindwa kabisa kutengeneza mifumo ya kuhifadhi maji itakayowawezesha wakazi wa Dar es salaam kutumia maji hayo walau hata mwaka mzima bila kusuasua?

Nashindwa kuwaelewa kabisa hawa DAWASA kipindi cha msimu wa mvua mnaacha maji yanapotea, then kipindi cha kiangazi mnatusumbua na mgao wa maji, mkiulizwa mnasema mpo katika matengenezo na bla bla kibao hivi mmeshindwa kuwa hata na matanki makubwa kwa ajili ya kuhifadhi akiba ya maji kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kama vile maziwa, mito mvua, visima n.k?

Soma Pia: Waziri wa Maji ingilia kati DAWASA, hali ya maji Dar ni mbaya sana

Hivi ninyi mnaojiita sijui wakurugenzi huko DAWASA mkikaa huko ofisini mnawazaga nini na kila mwezi mnadai ankara za maji tukishindwa kulipa mnakata chap ila huduma zenu ni mbovu mno... Aahh
 
Ukienda Mbezi beach ndio utajua uzembe wa Dawasco
 
Back
Top Bottom