KERO DAWASA, watu wa Mbezi Luis Makabe mpaka kwa Robert hatuna maji yapata wiki sasa. Mhandisi hapokei simu, namba ya huduma kwa wateja haipatikani

KERO DAWASA, watu wa Mbezi Luis Makabe mpaka kwa Robert hatuna maji yapata wiki sasa. Mhandisi hapokei simu, namba ya huduma kwa wateja haipatikani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

DegaMan

New Member
Joined
Mar 5, 2024
Posts
2
Reaction score
0
Sisi wakazi wa Mbezi Luis, Njia panda Makabe mpaka kwa Robert tunakaribia wiki sasa hatuna maji na hakuna taarifa rasmi yoyote toka kwa mamlaka husika. Tumekuwa tukinunua maji kwenye magari na bill imetoka kwa kiwango kilekile ingawa kwa mwezi wote huduma ya maji imekuwa ikisuasua.

Tunaomba mamlaka husika itoe ufafanuzi.
 
Hivi kuna waziri mjanja mjanja kama huyu wa maji,kero ya maji huwa ni kubwa ni vile watu tumeamua kuchimba visima vyetu lakini laiti tunekuwa tunategema mamlaka kutoa huduma ,hali ingekuwa mbaya sana
 
Dawasa wajifunze kwa ndugu zao Wa - Tanesco..kwenye masuala ya huduma kwa wateja.TANESCO siku hizi inajitahidi sana, simu wanapokea.huku mijini kuna magroup ya watsap ya wateja..unaandika kitu watu wanajibu...inatia moyo kidogo.

SASA hawa ndugu zetu DAWASA hawa...wanafanyakazi kama halmashauri kabisa...Wanachojua wao ni kusoma mita na kutoa bili, lkn uwaite sijui bomba limepasuka sehemu, my friend..mpaka waje...si mchezo, uwataarifu uharibifu wa mita...mpaka waje..utasubiri sana n.k hawa watu wajifunze kwa Tanesco..ofisi nzima ziwe karibu na watu..
 
Back
Top Bottom