Daz Baba: Msanii mkongwe aliyepotea kwenye game, lakini kazi zake bado hazichoshi kuzisikiliza!

PROF NDUMILAKUWILI

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2016
Posts
10,518
Reaction score
13,144
Dazbaba au daz mwalimu, huyu msanii alifanya poa sana miaka ya nyuma kidogo akiwa na kundi la Daz Nundaz vilevile alifanikiwa kufanya kazi zake mwenyewe zilizo fanya poa sana kwenye media tofauti na kuangusha albamu yake ya ELIMU DUNIA iliyofanya poa sana sokoni iliyokuwa na nyimbo kama Nipe tano, wife, mrembo namba 8 na ngoma zingine ambazo pia zilifanya poa sana.

Kwa kipindi cha mda mrefu sasa yuko kimya sana huyu jamaa lakini kazi zake kiukweli huwa hazichoshi kuzisikiliza ngoja tusubiri labda anaweza kurudi tena kwenye game tuka pata ngoma kali kama zamani kutoka kwake!

 
Ukimwoma live daz baba live, unaweza ukalia, nilimwonaga kkoo na maeneo ya kwetu pazuri Tabata
 
Nafikiri nshakuwa MTU mzima mi, sasa nahitaji mlembo wa kuishi nami , kuzaa na kulea watoto nami kwenye shida na raha avumilie nami, ..R.I.P Ngwair,Daz Nyimbo zake huwaga hazichoshi kusilikiliza .. Wife ndo no 1 kwangu
 
Kwenye hiyo album yangu bora kabisa kuwahi kutokea kuna nyimbo mbili sijawai kuzichoka.

Mwalimu na rastaman
 
Namuonaga segerea.....Poda ni kitu kibaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…