Dazzle camouflage: Michoro katika jezi ya tatu ya Manchester United

Jiwe_Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2018
Posts
416
Reaction score
807
Kuna kitu kimoja kuhusu hii jezi. Mchoro wa hii jezi unaitwa Dazzle Camouflage.

Dazzle camouflage ni mchoro ambao ulikuwa unatumika kwenye vita vikuu vya kwanza vya dunia.

Dazzle camouflage kwenye meli za Kivita ilikuwa inachorwa kwa kumaanisha hao ni MA - FIGHTER , WANA SPEED , HAWAPIGWI OVYO.

Wenzetu kibiashara kila kitu huwa kina kuwa na theme au meseji ya kibiashara.

Meseji ambayo wateja wengi huwa wananunua kwa ajili ya kunimotivate n.k.

Wenzetu hawauzi bidhaa wanauza feelings iliyopo ndani ya bidhaa.

Feelings zinazowekwa kwenye bidhaa ndiyo huwa zinanunuliwa.

Mtu ananunua feeling ya NIKE na siyo kiatu pamoja na kwamba kiatu kinaweza kikawa kizuri lakini ile feelings ya JUST DO IT inanunuliwa sana.

NDIYO maana asilimia kubwa ya Campaigns za Nike ni kuhusu na ujumbe wao wa Just Do It na siyo Campaign za kutangaza mchoro wa kiatu.

Watu wana focus kwenye kuuza na kununua feelings iliyopo ndani ya bidhaa.
Turudi kwenye hii Dazzle camouflage. Kwanini Nike walifanya vyema kwenye design ya Dazzle camouflage ? kwenye viatu na jezi ya timu moja huko Marekani ?Walichukua meseji ya Dazzle camouflage ( FIGHTER , SPEED , UNBEATABLE ) afu wakachanga na yao ile ya Just Do It .

Wakawezeka kutuambia Just Do It kwa sababu wewe ni fighter , una speed ya kukimbilia mafanikio na uko unbeatable.
Watu wanatumia aspirations na siyo price na uzuri kuuza jezi zao.Adidas baada ya kuona hivo wakacop design ya dazzle camouflage.

Lengo lile lile kuichukua meseji iliyopo kwenye Dazzle Camouflage. Meseji ambayo ilikuwa inatumika kwenye vita kuu vya kwanza vya dunia.

Meseji hii itafanya kuuza jezi nyie dunia ya tatu mtalalamika kuhusu ubaya wa jezi lakini dunia ya kwanza kwenye soko la Adidas watakuonesha namna ya kuuza feelings za hizi jezi ambazo sisi tunasema ni mbaya.
 
Mbona jezi iko poa kwa ajili ya kung'olea mademu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…