DBA - Doctor of Business Adminstration TCU munaitabua hiyo ? (Dual Masters Degree)

Mimi sio mdau wa TCU, lakini kwa namna nivyofahamu ni kwamba PhD na Doctor of something, zote zina rank sawa kwa kuwa ni doctorate degrees. Tofauti ni ndogo sana na hivi mstari unaozitenganisha sio rahishi sana kugundua. Hata hivyo utafiti unaofanywa katika Doctor of say science, Law, Education huwa ni lazima uwe ni problem/action oriented. Wakati PhD sio lazima ila inatoa mchango katika knowledge ya jambo fulani. Tukumbuke Tanzania kuna watu kama akina Mwakyembe ambao hawana PhD ila walitunukiwa Doctor of Juris yaani Doctor of Laws, kuna wengine wengi waliopata Doctor of Education, Doctor of Literature, etc. Kwa Tanzania ni ESAMI peke yao wanaotoa DBA yaani Doctor of Business Administration.

Hitimisho ni kwamba Doctor of Business Administration (DBA) na PhD in Business Administration zina level sawa kwa kuwa zote ni doctorate degrees. Isipokuwa suala la kutoa double masters ikawa sawa na Doctor of Business Administration lina utata, kimsingi na sidhani kwamba ni sahahi kuzichukulia hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…