DC Chuachua: Marufuku magari yanayofanya matangazo ya misiba jijini Mbeya

Hii ni kali. Sijawahi kusikia sehemu nyingine. Siyo tabia nzuri hata kidogo. Msiba siyo kitu cha kupitisha matangazo kama hayo hasa kipindi hiki ambacho kuna njia nyingi za mawasiliano
Ni Mila zao Sema waandishi wetu wajinga wangeweza tengeneza documentary kali

Ni hivi mtu akifa hospital gari hupita ikitangaza mitaani kuwa eg Mwakiyelelelewa aliyekuwa .... Wanataja wasifu kafariki msiba leo msiba uko mahali Fulani

Wakienda kufuata maiti mfano hospital pia gari hupita ikitangaza Sasa ndio tunaenda kuchukua mwili wa marehemu kupeleka uliko msiba

Wakishabeba kupeleka ulipo msiba gari inapita inatangaza Sasa ndio tumebeba mwili wa Marehemu Fulani kwenda nyumbani uliko msiba

Wakiondoka kusafirisha au kuzika gari hutangulia ikitangaza Sasa ndio tunaenda na marehemu kumsafirisha au kuzika kwao au makaburi ya mahali Fulani
Ni desturi zao anyway akina Pascal Mayala wangekuwa Kama waandishi wa CNN wangetengeneza documentary lakini waandishi wetu wengi Ni just reporters wa habari tu hawana Cha ziada

Sidhani Kama Ni sahihi kuzuia watu na desturi zao
 
Hata Mimi Sijaelewa kabisa ..sijui ya natumika maneno Gani pale!...Msiba...Msiba....,Usafiri utakuwepo...Na Chakula Cha kutoshaa...etc????!!!
Ni simple tu mfano " Na sasa mwili wa mpendwa wetu nyampanaga unapelekwa katika makazi yake ya milele kwa ajili ya maziko, kwaheri ndugu, jamaa,marafiki,,watoto na woteee tuliokusanyika mahali hapa". Huo ni mfano tu hakuna cha msiba,,,msiba,,,
 
Siku ya kwanza nilidhani ni msiba wa kiongoz wa nchi. Kumbe ni utaratibu wao watu wa Mbeya. Mtu hata kama aliumwa na alikosa hela ya dawa siku ya msiba lazima kuwe na bajet ya gari la mziki pamoja na MC. Mbeya ni jiji ila lina mambo ya kienyeji sana
Aisee kwa mtindo huo sikuchoshana tu watu na kelele za msiba zisizo husu watu wengine
 
Huko mbeya bado Kuna u primitive sana aisee I'm sorry to say this.
 
Huyo mkuu wa Wilaya ni mjinga. Kama angekuwa na akili angenukuu sheria inayoharamisha au government standing order, na siyo kuropoka tu.

Rais anawaokota jalala gani watu wa namna hii?
 
akisema yamekuwa yakileta hataruki kwa wananchi na kujenga hofu.
Kwa hiyo anataka Wananchi washtukie tu wameshakufa?

Taharuki ni muhimu ili Viongozi watafute Solution.

Taharuki akili hiyo
 
Aisee kwa mtindo huo sikuchoshana tu watu na kelele za msiba zisizo husu watu wengine
Wala sio kuchoshana, sisi wenyeji tumeshazoea ni utaratibu wetu, DC ametukosea sana yani kakurupuka

Cariha hujawahi fika Mbeya lakini thread zote zinazohusu Mbeya upo negative kinoma
 
Asante sana kwa contribution. Kumbe ni kitu kilichozoeleka. Wameanza tangu lini?
 
Matangazo haya unaletewa moja kwa moja na Mc dani fm, wakati huu tukielekea kumpuzisha mpendwa wetu pale kijijini ipinda,
 
Wala sio kuchoshana, sisi wenyeji tumeshazoea ni utaratibu wetu, DC ametukosea sana yani kakurupuka

Cariha hujawahi fika Mbeya lakini thread zote zinazohusu Mbeya upo negative kinoma
Utashangaa huyo Carina ni mshamba kutoka Shinyanga huko,Geita,Mtwara,Songea huko au sehemu nyingine ya kipumbavu wanakotumia punda kama usafiri.
Kisa amewahi fika Dara anashinda JF kuitukana ardhi takatifu ya Mbeya.
Jinga.
 
Viongozi wakifariki huwa tunaoneshwa hadi live kwenye tiviiii...inaleta taharuki sana kwa wagonjwa wanaokuwa mahospitali yenye tiviii
 
Yanakuudhi nini kwanini usifate mambo yako? Mjini kila mtu yupo huru kufanya atakacho. Unajua huo utaratibu Mbeya ulianzaje? Kwanini mikoa mingine hawafanyi hivyo?
Sasa unapowatangazia jiji zima kuwa umefiwa Wengine inawahusu nini?
 
Namuunga mkono kwa 101% . Tabia hii siipendi na inanikela sana. 2 weeks ago nilikuwa huko gari linatangaza msiba halafu linaenda speed 10 na kusababisha foleni kubwa. Mbeya yenyewe barabara moja tu.
Mjomba angu alifariki 2017 wakasema lazima tukodi gari la matangazo kwa 200,000/= wakati matibabu walikuwa hawachangii, shenzi sana. Nilipingana nao Sana but walinizidi nguvu hasa kwa kuwa mimi sio ukoo wao hata kama tiba mimi ndio nilihusika sana tu.

Huo utaratibu shenzi kabisa unakuta magari ya matangazo yametawala barabara halafu speed 10 watu wote inabidi muheshimu msiba.

Yaani wamechelewa Sana kukataza
 
Siku ya kwanza nilidhani ni msiba wa kiongoz wa nchi. Kumbe ni utaratibu wao watu wa Mbeya. Mtu hata kama aliumwa na alikosa hela ya dawa siku ya msiba lazima kuwe na bajet ya gari la mziki pamoja na MC. Mbeya ni jiji ila lina mambo ya kienyeji sana
Ni unafiki tu.unakuta mijitu mizima inakisanyana hospital hata kutoa hela ya kununulia dawa haitowi.akifa matangazo mji mzima. ni ushamba uliyopitikiza.
 
kunakua na msafara wa maiti na magari kibao kutoka mochwari hadi mahali pa maziko

zinapigwa nyimbo kwa sauti ya juu za maomblezo huku gari zikipita kwa madaha,wafiwa wamevaa sare na wamepanda kwenye magari yao kwa raha zao
Asante kwa ufafanuzi, lakini mfano kukiwa na misiba mitatu hali ya foleni inakuwaje kama ndo msafara mwendo wa madaha?!
 
Asante sana kwa contribution. Kumbe ni kitu kilichozoeleka. Wameanza tangu lini?
Miaka mingi sio leo Wala Jana .Ni desturi yao sijui mwaka gani lakini iko miaka

Na wakazi hawana shida nayo .Mnyakusya akifa Ni kawaida yao kuuliza maswali kibbao kuwa aliyekufa nani anatoka ukoo gani alikuwa Nani nk halafu hutungua kilio wakijua Ni wa kwao

Maiti huwa hawapendi kuipitisha kimya kimya

DC kawakosea watu wa Mbeya Ni Kama pwani uswahilini ukikuta watu wamefunga turubai katikati ya barabara wamefiwa hutakiwi kuwabughudhi Wala kuuliza mna kibali Cha kuweka turubai au kufunga barabara tafuta njia nyingine wao mtaa mzima Wala hawana shida

Tatizo Ni hao watu wa kuja toka mikoa mingine wanaona Ni public nuisance.Ukifika kwa watu wewe DC heshimu desturi za watu hata weather ukifa matangazo yatakuwa kila Kona ndio maana hata Raisi akifa radio na TV zote huwa Ni kutangaza kifo tu

Huyu DC baadaye atadai kuwa watu wakienda kuzika makaburini waombe kibali Traffic wakibeba jeneza kwenda kuzika mabegani wakiwa wanatembea barabarani sababu barabara Ni ta magari si ya watembea kwa miguu wabeba jeneza kwenda makaburini

Kuna vitu kiongozi anatakiwa kupotezea sio kila kitu unachonga mdomo tu
 
Wala sio kuchoshana, sisi wenyeji tumeshazoea ni utaratibu wetu, DC ametukosea sana yani kakurupuka

Cariha hujawahi fika Mbeya lakini thread zote zinazohusu Mbeya upo negative kinoma
Acheni mila za kale kwanza mnachafua mazingira misiba wenu unahusu nini wengine jamani.
 
Utashangaa huyo Carina ni mshamba kutoka Shinyanga huko,Geita,Mtwara,Songea huko au sehemu nyingine ya kipumbavu wanakotumia punda kama usafiri.
Kisa amewahi fika Dara anashinda JF kuitukana ardhi takatifu ya Mbeya.
Jinga.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]shanyanga kwetu hatuwezi fanyia msiba promotion kwani unaleta hela mezani, imagine daily taarifa za msiba hata haukuhusu sikuchoshana huko na hayo matangazo jamani. Ndo naskia msiba unakuwa na promotion za kuzungushwa kitaa naona DC yuko sahihi kwa Hilo katazo
 
Utashangaa huyo Carina ni mshamba kutoka Shinyanga huko,Geita,Mtwara,Songea huko au sehemu nyingine ya kipumbavu wanakotumia punda kama usafiri.
Kisa amewahi fika Dara anashinda JF kuitukana ardhi takatifu ya Mbeya.
Jinga.
Hahaha cariha ni manka mzee, mjeuri sana ila nimempicture atakuwa demu flani class hivi 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…