DC Chuachua: Marufuku magari yanayofanya matangazo ya misiba jijini Mbeya

Acheni mila za kale kwanza mnachafua mazingira misiba wenu unahusu nini wengine jamani.
Mkuu hakuna ishu ya ukale wala usasa, gari ya matangazo ni mazoea halafu huwa haileti jam kama waongeza chumvi wengi walivyochangia hapo


Halafu Mbeya sisi tunajuana maeneo mbali mbali, gari ya matangazo husaidia pia kutoa taarifa kwa wale ambao hawajapata
 
Huwa yanaudhi sana. Namsapoti 100%

Ujinga unashabikia. Au kwa vile wanatumia magari. Ninatoka usukumani, misiba hutangazwa kwa jembe tena siku hizi ni kwa bodaboda.

Kutaarifu msiba imekuwa na sisi siku nyingi. Wewe huenda ni mtoto. Watu wazima watakumbuka RTD (Radio Tanzania Dar es Salaam) walikuwa na taarifa za misiba kwa dakika 5 mara baada ya taarifa ya habari saa 2 usiku (prime time)!!

Hata usipotangaza msiba, taarifa za msiba zitasambaa au kutokana na umaarufu wa marehemu, au ukaribu wa marehemu na watu maarufu.

Unasemaje sasa kuhusu misiba ya wakuu wa mikoa, mawaziri na wakubwa wa nchi kupitia runinga?? Nayo waache??

Crap!! Nchi ya kushughulika na vitu vidogo vidogo huku vya maana tukiviweka kando!
 
Kula like mkuu, huu mfumo wa elimu ya mzungu unafanya waafrika tukatae vyetu kwa kisingizio cha ukale

Mimi kama mwanambeya sioni tatizo lolote kuhusu magari ya matangazo, DC katukosea
 
Nchi yetu ina tatizo moja. Inaongozwa kwa kauli za wanasiasa. Sheria, kanuni na miongozo yote imelala. Ni kama haipo. Wanasiasa ndiyo wamegezwa kuwa sheria, kanuni na miongozo. Tunaongozwa kama watoto wa chekechea. Watoto wa chekechea ndiyo husimamiwa kwa kuongozwa.
 
Huu utetezi mwepesi sijawahi ona yani matangazo ya wafu ni kukosesha watu amani moyoni bana, Mimi sikubaliani nayo kijijini kwetu hata kulia kwa mayowe huwa hamna hicho kitu sikuhizi.
 
Hii ni kali. Sijawahi kusikia sehemu nyingine. Siyo tabia nzuri hata kidogo. Msiba siyo kitu cha kupitisha matangazo kama hayo hasa kipindi hiki ambacho kuna njia nyingi za mawasiliano
Kwa tamaduni zenu ni suala zito lakini kwa jamii zingine ni la kawaida tu tusilazimishe watu waishi kwa tamaduni ambazo siyo za kwao
 
Huyo mkuu wa wilaya anasema wenye magari wanazua taharuki wakati sio kweli yeye ndie anasua taharuki wana Mbeya Mjini hawaoni taharuki magari yakipita yakitangaza ila yeye kuzuia ndio analeta taharuki

Aulize mwenzie Chalamila aliyekuwa mkuu wa mkoa mbabe kupinga desturi hizo sababu kwao hazipo Sasa hivi Ni mkuu wa mkoa tena? Ukifika kwa watu heshima Mila na desturi zao usijifanye mjuaji kupitiliza kisa tu umeteuliwa na Raisi
 
Dizaini kama wanaalika watu ili wakaongeze mzuka wa kulia msibani,ukiudhuria msiba wa mnyakyusa utastaajab na kuburudika wale watu wanajua kulia bana loh!!πŸ˜†
 
Asante kwa ufafanuzi, lakini mfano kukiwa na misiba mitatu hali ya foleni inakuwaje kama ndo msafara mwendo wa madaha?!
Kuna wakati pale mwanjelwa Jam imeshika na hapo inapishana misiba, harusi na graduation. Mbeya mpaka graduation za darasa la saba wazazi wanawakodia watoto magari ya mziki wanavalishwa sare wanapitishwa mitaani na ukumbi wa sherehe wanachukua
 
Huyo mzee DC namjua vizuri kumbe kapelekwa huko Mbeya,Ngoja nimpigie simu atengue kauli yake.
 
Kwa hiyo hapo huyo mkuu wa wilaya ndio katatua kero za walio wengi hapo Mbeya mjini?

Huo ndio ubunifu wa juu was kutatua kero za wanna Mbeya Mjini? Kuwa kero kuu ya wanambeya mjini ilikuwa matangazo ya magari ya msiba?

Jamani haya hiyo ndio kazi iendelee?
 
Kuna wakati pale mwanjelwa Jam imeshika na hapo inapishana misiba, harusi na graduation. Mbeya mpaka graduation za darasa la saba wazazi wanawakodia watoto magari ya mziki wanavalishwa sare wanapitishwa mitaani na ukumbi wa sherehe wanachukua
Hahahaha, Mbeya nawasalimia sana! Kwa kweli mmetisha daa!
 
Yaaan msiba billa kuwa na mziki na gari ya matangazo huku mbeya ni Kama kukiuka utamaduni we2 na Kila jamii Ina utaratibu wake kama walivo wale jamaa wa kule nchini ghana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…